Jaji mstaafu wa mahakama ya rufaa nchini tanzania mama EUSEBIA MUNUO ambaye alikuwa ndiye mkufunzi katika mafunzo hayo yaliyoendeshwa leo jijini Dar es salaam |
Rushwa ya ngono pamoja
na matumizi mabaya ya madaraka yametajwa kuwa ni moja kati ya matatizo makubwa
ambayo yamezidi kuweka mizizi nchini tanzania na kuwaadhiri wasichana wengi
huku sheria ikishindwa kuweka wazi adhabu mahususi ili kuwabana wanaohusika katika
swala hilo.
Hayo yamesemwa leo
jijini dare s salaam na Jaji mstaafu wa mahakama ya rufaa nchini tanzania mama
EUSEBIA MUNUO wakati akiendesha mafunzo maalumu kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha
Dar es salaam mafunzo yaliyolenga kuzungumzia madhara na jinsi rushwa ya ngono
inavyoathiri kizazi kukubwa cha wasichana wa sasa nchini tanzania.
Wanafunzi mbalimbali kutoka chuo kikuu Dar es salaam waliohudhuria katika mafunzo hayo leo jijini Dar es salaam |
Amesema kuwa tatizo la
ruswa ya ngono limekuwa likiongezeka siku hadi siku nchini kutokana na kutokuwa
na sheria mahususi ambayo inawaadhibu moja kwa moja wahusika katika swala hilo.
Amesema kuwa wasichana
wengi wanapokuwa katika harakati za kutafuta ajira katika maofisi mbalimbali
wamejikuta wakitumia miili yao kuwashawishi mabosi wao ili waweze kupata ajira
jambo ambalo amesema kuwa sio sahihi na wasichana hao wamekuwa wakikosa msaada
kuhusu swala hilo.
Amesema kuwa hata katika maofisi mbalimbali
kumekuwa na wasichana ambao hawana vigezo vya kuwa katika maofisi hayo ila wapo
tu kwa sababu wanatembea na mabosi wao jambo ambalo limetajwa kuleta madhara
makubwa ikiwemo kushusha ufanisi wa kazi pamoja na ofisi husika kwa ujumla.
Mwanafunzi CATHERIN OLOMY akizungumza na mwandishi wa mtandao huu juu ya mafanikio ya semina hiyo ya siku moja kwao na kwa jamii kwa ujumla |
Baadhi ya wanafunzi
ambao wamehuduria mafunzo hayo ya siku moja ambayo yameandaliwa na WLAC kwa
kushirikiana na TAWLA mwanafunzi
CATHERINE OLOM
Y ambaye ni mmoja ya washiriki anasema kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwa wanafunzi wa sasa hususani wasichana kwa kuwa yatawasaidia kujiamini kujua haki zao kama wanafunzi na watoto wa kike,ikiwa ni pamoja na kujua uthamani wao pindi wanapokutana na swala la rushwa ya ngono.
CATHERINE OLOM
Y ambaye ni mmoja ya washiriki anasema kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwa wanafunzi wa sasa hususani wasichana kwa kuwa yatawasaidia kujiamini kujua haki zao kama wanafunzi na watoto wa kike,ikiwa ni pamoja na kujua uthamani wao pindi wanapokutana na swala la rushwa ya ngono.
No comments:
Post a Comment