Wednesday, April 29, 2015

UMESKIA NCCR KUJITOA UKAWA--TAARIFA MPYA HII HAPA

VIONGOZI  wa Vyama Vikuu vya Upinzani vinavyounda (UKAWA) Vimekanusha Uvumi unaoenezwa na Vyombo vya Habari kuwa Miongoni mwa Chama cha siasa kinachounda umoja huo ambacho ni NCCR Mageuzi  kwamba kimetoa hoja ya kujitoa kwenye umoja Huo, na  kusema huo ni upotoshaji Wa Vyombo vya Habari ambavyo vinatumiwa na Chama cha Mapinduzi CCM.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
        
Kauli hiyo ya (UKAWA) inakuja ikiwa ,Gazeti la moja linalotoka kila siku Gazeti la Mtanzania toreo la leo Tarehe 29-mwezi wa nne mwaka huu bila ya kutaja chanzo cha uhakika kimeripoti Habari kwamba Vyama hivyo vikuu vya Upinzania vimeshindwa kufikia muhafaka kwenye ugawaji wa Majimbo  na kudai kwamba Chama cha NCCR mageuzi kimepeleka hoja ya kujitoa kwenye Umoja huo.
         
 Wakikanusha taarifa hizo leo ,wakati wakizungumza na  Mtadao huu kwa Nyakati Tofauti  viongozi wa Ukawa  unaoundwa na  Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD wameonyesha kusikitishwa na Taarifa wanaodai ni ya kuzushi na zenye uwongo na kushangaa kuripotiwa kwenye 
Gazeti ambalo wanasema limejaa wahariri mahiri nchini.
        
Wa kwaza kukanusha Taarifa hiyo ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dokta Wilboard Slaa  ambapo amesema taarifa hizo zinalengo la kuwavunja nguvu Watanzania kulekea kipindi hiki anachodai wanakwenda kushika Dola.
     
     “Nashangaa sana hicho kigazeti kuandika Taarifa ya uzushi kama hiyo,wakati ukweli ni kwamba kwa sasa tumefikia asilimia 84 ya makubaliano ambayo tunakwenda vizuri sana na tena tupo kamili kuhakikisha tunautoa utawala huu mbuvu wa CCM,leo anakuja mtu kwa kutumiwa huko anakuja na taarifa za uongo kama hizo”Amesema Dokta Slaa.
         
 Dokta Slaa ameongeza kuwa hata Hoja ambayo wanasema kwa Chama mwenza wa Ukawa ambao ni NCCR Mageuzi kutoridhika na Ugawaji wa Majimbo ya Ubunge kwenye Uchaguzi wa hapo baadae na kusema kwamba wala kwenye Kikao kilichofanyika jana Jijini hapa ambacho pia leo kinaendelea, wala hakijavunjika na wala chama cha NCCR hawajasema wataka kujitoa.
          
 “Kwanza kikao cha Jana tulichokutana na Viongozi wenzetu wa Ukawa hakijavunjika kama wanavyodai kwani hiyo hoja ya Ugawaji wa Majimbo hatujazungumzia kwenye kikao hicho,kwani siku nzima tulizungumzia namna ya kupata vyanzo vya pesa ili tuweze kufanya Kampeni nchi nzima sasa huyo mwandishi wa Habari katoa wapi Taarifa hizo”ameendelea kusema Dokta Slaa.
    
  Mwandishi wa Mtandao huu alipumuuliza ni Majimbo gani ambayo wanashindwa kufikiana,Dokta Slaa amesema hawezi kujibu swali hilo kwani hayo ni mambo ya ndani ya Umoja huo na akawataka Watanzania kuwa na subira wakati viongozi hao wakiweka mambo sawa na kudai UKAWA watatoa wagombea Bora ambao anazidi dai watahakikisha wanaitoa CCM Madarakani.
         
Kwa upande wake Mbunge wa Kigoma Kusin David Kafulila ambaye pia ni Mjumbe wa kamati kuu ya NCCR-Mageuzi naye amekanusha taaria hizo kwamba Chama hicho kimepeleka hoja za kujitoa kwenye UKAWA.

“Kiukweli mimi nashangaa taarifa za upotoshaji kwenye Gazeti kama hilo,wakati ukweli ni kwamba UKAWA  tumefikia asilimia 84 ya makubaliano  na wenzetu,eti leo tujitoe,maana sisi tutakuwa watu wa ajabu sana ukweli ni kwamba hatujawai peleka hoja hizo na vilevile,tupo kwenye asilimia za mwisho”amesema Kafulila.
      
  Mbunge Kafulila amebanisha kuwa kwa sasa umoja huo unaweka mipango ambayo anasema ni mizuri ya kuhakikisha kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi Mkuu hapo baadae na kuwataka Watanzania kupuuza Taarifa ambazo anaziita ni za kizushi.

         Naye Kiongozi Mmoja wa Juu wa Chama cha Wananchi CUF  aliyezungumza na Mtandao kwa sharti la kutotaja jina lake kwenye mtandao huu ambapo amfichua siri ambayo anasema kwa sasa Chama cha Mapinduzi  CCM kimepeleka Fungu la pesa kwa waandishi wa Habari pamoja na Wahariri kuandika Habari za upotoshaji juu ya UKAWA ili kuwapa hofu wananchi na hata alipoiona Taarifa hiyo kwenye Gazeti la Mtanzania amedai kuwa hakuweza shangaa.

No comments: