Sunday, May 31, 2015
SOMA SAENTENSI 23 ZENYE MATUMAINI ALIZOTOA NCHEMBA WAKATI AKITANGAZA NIA YAKE
DIWANI WA CCM AWASHUKURU MABALOZI KATIKA KATA YAKE KWA KAZI KUBWA WANAYOFANYA
Diwani wa kata ya
Ndugubi iliyopo katika Jimbo la Kinondoni mh CHARLES MGONJA leo amekutana na
mabalozi wote waliopo katika kata yake kwa lengo la kuwakutanisha kwa pamoja
kujadili kuhusu kazi ambazo zinafanywa
na diwani huyo pamoja na kuwashukuru madiwani hao kwa kushiriki kikamilifu
katika ujenzi wa mambo ya maendeleo katika kata hiyo.
Akizungumza na mwandishi
wa mtandao huu nje ya mkutano huo amesema kuwa kumekuwa na malalamiko kutoka
kwa mbalozi hao kuwa wamekuwa hawapati nafasi kama hiyo ya kukutana na kujadili
kwa pamoja na viongozi walio juu yao pamoja na kazi kubwa wanayoifanya,jambo
ambalo limemsukuma kuwakutanisha mabalozi hao kujadili kwa pamoja na kuelewa
kila kitu ambacho serikali yao inakifanya katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Mabalozi mbalimbali waliojitokeza katika kikao hicho |
Amesema kuwa ufanisi wa
kiongozi wa ngazi za juu za serikali hauwezi kuwa na maana kama hauna mahuziano
mazuri na viongozi wa ngazi za chini za wakiwemo mabalozi hao kwani ndio
wanaohakikisha kuwa katika mitaa yote kunakuwa na ulinzi wa kutosha na
kuimarisha amani katika maeneo yote ya kata hizo.
TIGO YADHAMINI MASHINDANO YA MBUZI DAR ES SALAAM
|
Vijana wakiingiza Mbuzi katika eneo la kukimbilia wakati wa tamasha la mbio za Mbuzi (Goiat Race) lilofanyika jijini Dar es Salaam |
|
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo John Wanyancha akikabidhi hundi kwa mmiliki wa Mbuzi aliyeshinda, Mark Golding kutoka kampuni ya PM Group |
TIZAMA ALICHOKIFANYA TENA DK SLAA ZIARA YAKE
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA MARIAN BAGAMOYO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015. Picha na OMR
|
WASIRA ALIPUKA,AMPIGA KIJEMBE KIAINA LOWASA,ATANGAZA NIA YA KWENDA MAGOGONI
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, amnabe pia ni Mbunge Bunda mkoani Mara, Steven Masato Wasira leo ametangaza rasmi nia yake ya kuwania urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu utakaofanyikia baadae mwaka huu.
Katika hotuba yake ya takribani dakika 60 mh WASIRA ametumia muda mwingi kukemea vitendo vya rushwa hiuku akiwahmiza wananchi kumchagua kiongozi ambaye hatawaibia mali zao na badala yake wamchague mtu ambaye atawatumikia watanzania.
Saturday, May 30, 2015
PICHA 50-ALICHOKIFANYA LOWASA HUKO ARUSHA LEO ZIKO HAPA
Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola akisalima umati wa watanzania uliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, kumsikiliza Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa (kulia).
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa, kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo.
TIZAMA DK SLAA ALIVYOANZA ZIARA YAKE,AKABIDHIWA UCHIFU
TIZAMA ATAKAPOSIMAMA LOWASA LEO KUZUNGUMZA NA WATANZANIA
Friday, May 29, 2015
WAISLAM--HATUHUSIKI HATA KIDOGO NA UGAIDI UNAOENDELEA AFRICA,SOMA HII
Imeelezwa kuwa vitendo
vya ugaidi na mauaji yanayofanywa na watu mbalimbali barani Africa na duniani kwa ujumla hayahusiani hata
kidogo na dini ya kiislam kama ilivyokua ikielezwa na wadau mbalimbali kuwa
mauaji hayo yanahusiana na imani ya dini ya kiislam.
Kauli hiyo imetolewa
leo jijini Dare es salaam na kiongozi Mkuu wa kiroho wa Waislam Dhehebu la SHIA
ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA wakati akizungumza katika kikao cha
pamoja cha viongozi wa dini zote kikao kilichoandaliwa na chuo cha kidini cha
IMAM JAFAR SWADIQ,kigogo Jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa ugaidi
katika bara la Africa umekuwa ukitafsiriwa kuwa ni jambo ambalo limekuwa katika
msukumo wa dini ya kiislam jambo ambalo amesema kuwa watanzania wanapaswa
kuelewa sio sahihi kuwatuhumu waislam kwa ugaidi kwani hakuna kitabu chochote
kinachoruhusu muislam kufanya mauaji kwa mwadamu mwenzake.
Amefafanua kuwa
mivutano na Ugaidi uliyopo barani Africa umekuwa ukisababishwa na mambo matatu
ambayo ameyataja kuwa ni ugaidi wa kifikra,kiuwezo na ugaidi wa kudai haki.
Wajumbe mbalimbali wakichangia |
Aidha Ameongeza kuwa
dini zote duniani hakuna hata ushaidi wa dini moja ambayo inaruhusu ama
kushabikia vitendo vya mauaji ya kigaidi yoyote yanayotokea afrika..
Katika hatua nyingine
sheikh JALALA akizungumzia swala ambalo limekuwa likitamkwa na serikali kuwa
viongozi wa dini ya kiislam wamekuwa wakiwafundisha vijana wao wa mbinu na njia
za ugaidi ameitaka serikali kuacha kauli hizo kwani ni kauli za kichochezo na
zisizo na ushahidi wowote na badala yake wafwatilie swala hilo kiundani pasipo
kuitaja dini yoyote kuhusika.
Akizungumza katika
kikao hicho muwakilishi wa wakiristo katika mkutano huo pastor PRINCE ERASTO
IKONGO kutoka pentecoste Tabata amesema kuwa viongozi wa dini za kikiristo
wamekuwa na hofu kubwa juu ya ndugu zao ambao ni waislam hofu ambayo
wamejengewa kuwa viongozi wa dini za kiislam pamoja na waumini wao ni watu wa
mauaji na ugaidi jambo ambalo amewatoa wasi wasi wakristo na kuwataka kujenga
umoja na mshikamano juu ya waislam na dini zote Tanzania ili kuidumisha amani
ya nchi.
Amesema kuwa hofu
iliyojaa miongoni mwa viongozi wa dini za kikristo ni hofu ambayo imejengwa na
wanadamu kuwa waislam ndio wanaohusika na mauaji mbalimbali ambayo yanatokea
duniani ya kigaidi jambo ambalo linapaswa kufutika miongoni mwa wakristo ili
waweze kudumisha umoja wanchi.
Kikao hicho kimefanyika
leo Jijini Dar es salaam Ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya wiki ya ukombozi
wa bara la Africa kilikua na kauli mbiu ya TUUNGANE KWA PAMOJA KUUPINGA UGAIDI
AFRICA ambapo kimehudhuriwa na viongozi kutoka dini zote huku lengo kuu la
kikao hicho likiwa ni kujadili kwa pamoja maswala ya ugaidi barani Africa na
kuona ni njia gani zinazoweza kutumika kuondokana na tatizo hilo.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA KUAPISHWA RAIS WA NIGERIA LEO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Asha Bilal, wakiteremka kwenye Ndege walipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Asha Bilal, wakiwasili kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na mtoto Ernest Nkayala alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea shada la maua kutoka kwa Mtoto Elin Mwandobo alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ngoma za kabila la Kinigeria alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ngoma za kabila la Kinigeria alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
(Picha na OMR)
TIZAMA RATIBA YA DK SLAA KUANZIA KESHO ANAVYOIZUNGUKA TANZANIA
Kupitia taarifa hii
kwa vyombo vya habari Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuujulisha
umma wa Watanzania kuwa Katibu Mkuu, Dk. Willibroad Slaa atafanya ziara ya
kikazi katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Mbeya, Rukwa na Katavi, ambapo atakuwa
na shughuli kadhaa, ikiwemo kukagua mwenendo wa uandikishaji wa wapiga kura
unaofanyika kwa mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR).
Thursday, May 28, 2015
TIGO NA HUAWEI ZATOA MSAADA WA KOMPYUTA 10 NA HUDUMA YA INTANETI KWA SHULE YA MSINGI CHUDA MKOANI TANGA
Meneja Mahusiano kwa Umma wa kampuni ya Huawei Jin Liguo akiongea na waandishi , Walimu na Wanafunzi wa Shule ya msingi Chuda wakati wa sherehe za kukabidhi kompyuta 10 zenye inteneti ya bure ya Tigo kwa shule hiyo iliyopo mkoani Tanga, Msaada huo ulitolewa na Kampuni ya Tigo kushirikiana na Kampuni ya Huawei. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani Goodluck Charles ,Mwalimu Mkuu wa Shule ya Chuda Omari Masukuzi na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Magalula Said Magalula.
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani Goodluck Charles akikabidhi msaada wa Kompyuta zenye intaneti ya bureya Tigo kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chuda Mkoani Tanga Bw. Omari Masukuzi hiyo ni moja kati ya kompyuta 10 zilitolewa na kampuni ya Tigo pamoja na Huawei kwa shule hiyo. Wanaoshuhudia wa pili toka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Magalula Said Magalula, Meneja wa Mawasiliano kwa Umma wa Huawei Jin Liguo na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe.Abdallah Suleiman.
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani Goodluck Charles akiongea na waandishi , Walimu na Wanafunzi wa Shule ya msingi Chuda wakati wa sherehe za kukabidhi kompyuta 10 zenye inteneti ya bure ya Tigo kwa shule hiyo iliyopo mkoani Tanga, Msaada huo ulitolewa na Kampuni ya Tigo kushirikiana na Kampuni ya Huawei. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa Tanga Mhe. Magalula Said, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Chuda Omari Masukuzi.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Chuda Mkoanin tanga wakipokea Kompyuta kwa niaba ya wenzao ambazo zilitolewa na kampuni za Tigo na Huawei.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo
Meneja Uwajibikaji kwa Jamii wa Kampuni ya Tigo Bi. Woinde
Shisael akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Magalula Said
Magalula na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe.Abdallah Suleiman wakati wa sherehe za
kukabidhi msaada wa kompyuta 10 kwa
shule ya msingi Chuda Mkoani Tanga leo
|
Mkoa wa Tanga Mhe.Magalula Said Magalula akiongea na waandishi , Walimu na Wanafunzi wa Shule ya msingi Chuda wakati wa sherehe za kukabidhi kompyuta 10 zenye inteneti ya bure ya Tigo kwa shule hiyo iliyopo mkoani Tanga
Mwalimu wa shule ya Chuda Bi.Teddy Simba akipokea simu kwa niaba ya wenzake toka kwa Mkoa wa Tanga Mhe.Magalula Said Magalula. Simu hizo zitawaweza walimu wa shule hiyo kuweza kuwasiliana wao kwa wao na kuperuzi intaneti bila gharama yeyote kwa kupitia mtandao wa Tigo.
Subscribe to:
Posts (Atom)