Imam mkuu wa msikiti wa AL-GHADIIR uliopo kigogo Jijini Dar es salaam imam HEMED JALALA akizngumza jana katika ibada hiyo |
Watanzania pamoja na waislam nchini wametakiwa
kuendelea kuitunza aman iliyopo nchini na kuidumisha kwani ndiyo zawadi pekee
ambayo mwenyezi mungtu zmeizawadia Tanzania.
Wito huo umetolewa
Jijini Dar es salaam na imam mkuu wa msikiti wa AL-GHADIIR uliopo kigogo
Jijini Dar es salaam imam HEMED JALALA wakati wa ibada maalum ya kumbukumbu ya
aliyekuwa imam maarufu na mpenda amani katika dini hiyo imam ALI ibada ambayo
ilifanyika Jijini Dare s salaam.
Amesema ni muda wa viongozi wa kiiislam na dini zote
kuungana kwa pamoja kuhakikisha kuwa wanaitetea amani ya nchini ambayo ipo
hatarini kutoweka kwani kinyume na hapo kunaweza kutokea matatizo makubwa sana
ambayo yamekuwa yakishughudiwa katika nchi nyingine duniani.
Aidha imam JALALA amesema kuwa tatizo kubwa
linalowakumba waumuni wa dini za kiislam ni ,kukosa umoja wa kuwa na kiongozi
mmoja au baba mmoja ambaye atawasimamia waislam katika shughuli za kiimaendeleo kama ilivyo
kwa dini nyingine jambo ambalo amesema
kuwa limekuwa likizuia waislam kupiga hatua katika maswala ya kimaendeleo kutokana na kukosa
mtetezi mmoja ambaye anaweza kuwasemea waislam wote.
Ibada hiyo maalum ilikuwa na lengo la kuienzi,kuidumisha
amani ya Tanzania kwa kile ambacho kimetajwa kuwa IMAM ALI alikuwa mstari wa
mbele kuhimiza aman duniani katika kipindi chake chote alichoishi .
No comments:
Post a Comment