Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Chamwino Ikulu, Joseph Seganje kuhusu Mnara wa kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliyeishi katika kijiji hicho, kuanzia Julai 10.1971 hadi Oktoba 30.1971 akihimiza siasa ya ujamaa na kujitegemea nchi nzima, wakati Waziri Membe alipofika wilayani Chamwino Mkoa wa Dodoma Juni 22.2015, kwa ajili ya kutafuta wadhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Wa pili (kushoto) ni Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Janeth Mashele.
|
No comments:
Post a Comment