Kikundi cha CHADEMA cha REDBRIDGED |
Dakika chache
zilizopita habari kutoka katika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ni kuwa
msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania Jaji MUTUNGI ametangaza kupiga
marufuku vyama ambavyo vinamiliki vikundi mbalimbali vya ulinzi na usalama kwa
kusingizia kuwa ni kwa ajili ya ulinzi wa vyama hivyo na kuvitaka kuvifuta mara moja kwani ni
kinyume na sheria za Tanzania kwa chama kumiliki kikundi ambacho kinapewa
mafunzo ya aina yoyote ya kijeshi.
Kikundi cha ccm cha GREENGUARD |
Amesema kuwa sheria za Tanzania
pamoja na katiba zinapiga marufuku kwa chama chochote cha siasa kiwe
kimesajiliwa au hakijasajiliwa kumiliki kikundi ambacho kitakuwa kinafanya kazi
sawa na jeshi la polisi au majeshi ya Tanzania ambapo amesema kuwa kwa mujibu
wa sheria hiyo jukumu la kulinda raia na mali zao linabaki kuwa la jeshi la
polisi Tanzania.
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi |
Amesema kuwa vikundi
hivi vilianzishwa wakati wa mfumo wa chama kimoja na vilikuwa ni vikundi vya
wanachama waliopewa jukumu la kuangalia ulinzi wa mali za chama husika,kulinda
viongozi na kupanga wanachama wakati wa mikutano ya kisiasa ambapo amesema kuwa
kipindi hicho wanachama hao walikuwa kama wanafamilia na hawakuwa wakipewa
mafunzo ya aina yoyote ya kijeshi kama inavyoonekana sasa katika vyama kadhaa
nchini Tanzania.
Aidha amesema kuwa
baada ya mfumo wa vyama vyingi vya siasa kuingia nchini Tanzania sheria hiyo
haikubadilika na badala yake waliamini kuwa vyama hivyo vingefwata shertia
zilizowekwa na nchi lakini badala yake imeonekana kukiuka sheria hizo.
Baadhi ya vyama ambavyo vinamiliki vikundi hivyo ni pamoja na ccm ambao wanakikundi cha greenguard,chadema na kikundi cha Redbridged,pamoja na chama cha wananchi cuf na kukundi cha blueguard.
No comments:
Post a Comment