Monday, June 15, 2015

DRFAYASIKITISHWA NA MATOKEO MABAYA YA TAIFA STARS.

Omary Katanga,mkuu wa habari na mawasiliano DRFA


Chama cha kandanda mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimesikitishwa na
matokeo mabaya iliyoyapata timu ya taifa (Taifa Stars) kwa kufungwa mabao
3-0 dhidi ya Mafarao wa Misri,katika mchezo wake wa kwanza uliopigwa jana usiku ugenini wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya kuwania kombe la mataifa ya afrika (AFCON).

Mwenyekiti wachama hicho,Almas Kasongo, amesema matokeo hayo
yamewafadhaisha mno watanzania wenye uchu wa kuona timu hiyo inapata matokeo mazuri yaliyokosekana kwa kipindi kirefu.

Amesema anaamini kuwa kikosi hicho kina wachezaji wazuri na wenye uwezo
lakini wamekuwa wakikosa mbinu za kufanya vizuri kwenye timu ya taifa hasa kwenye safu ya ushambuliaji,ikilinganishwa na uwezo wanaouonesha kwenye michuano ya ligi wakiwa na klabuzao.

Hata hivyo Kasongo amesema licha ya Stars kuanza vibaya katika harakati zake za
kuwania tiketi yamichuano hiyo ya afrika,bado nafasi ipo ya kujipanga upya
kwa kuanza kuangalia uwezo wa benchi la ufundi.

Aidha amesema DRFA inaamini kuwa Tff  inauwezo wa kutafuta mwarobaini wa
kutibu tatizo la matokeo mabaya kwa Starz,bila kumuonea mtu aibu.

……………………………………………….

ILALA, KINONDONI,ZAPONGEZWA MICHUANO YA TAIFA U-13.

Chama chakandanda mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimezimwagia sifa timu
za vijana za Ilala na Kinondoni zilizoshiriki katika michuano ya kuwania
ubingwa wa taifa chini ya miaka 13,ambapo fainali zake zimefanyika jiji Mwanza
mwishoni mwa wiki.

Katika michuano hiyo Ilala imetawazwa kuwa mabingwa wapya baada ya
kuikandamiza mabao 3-2 timuya Alliance,katika mchezo wa fainali,huku kikosi cha Kinondoni kikimaliza katika nafasi ya tatu.

Matokeo hayo yamepigiwa makofi na uongozi wa DRFA,na kuzitaka timu hizo
ziendee kukaza kamba ili kufikia mafanikio yanayohitajika katika medani ya soka
hapa nchini.

Mwenyekiti wa chama hicho,Almas Kasongo,amesema uwezo uliooneshwa na timu hizo zilizopo katika himaya yake kwa muda wote wa mashindano,zinatoa
taswira za kuwapata wachezaji wazuri wa baadaye kwenye vilabu mbalimbali vya
jijini Dar es Salaam na kwamba ni dira ya mkoa huo kuwa kitovu cha wachezaji nguli wa wakati ujao.

Aidha Kasongo ameipongeza Tff  kwa kuwepo na mashindano hayo ya ubingwa wa taifa kwa vijana chini ya miaka 13,na kuwataka wendeleze kwa nguvu zote
mipango waliyonayo yakuibua na kukuza vipaji vya soka kwa vijana.

IMETOLEWA NA DRFA,

Omary Katanga,mkuu wa habari na mawasiliano DRFA

No comments: