Kituo cha sheria na haki za Binadamu nchini Tanzania LHRC kimefanya mkutano wake mkuu wa 14 wa wanachama wake mkutano ambao umeambatana na muendelezo wa maadhimisho ya miaka 20 ya ufanyaji kazi wa kituo hicho ambayo kilele chake ni hapo mwezi September, mkutano ambao unafanyika Jijini Dar es salaam.
Mkutano huo ambao umehudhuriwa na wanachama mbalimbali kutoka kila kona ya Tanzania umefwatiwa na warsha iliyoendeshwa katika kituo hicho ya kujadili kwa pamoja na kuona changamoto mbalimbali ambazo wanahitaji kuzifanyia kazi ili ziweze kufikia malengo waliyojiwekea ya kuwasaidia watanzania wengi zaidi kutambua na kuzijua haki zao kwa kina.
Akizungumza na Mtandao huu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho Bi HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa Kituo hicho kilianziswa miaka ya 80 kwa lengo la kutoa msaada wa kisheria kwa watanzania ambapo amesema kuwa mwanzo Kituo hicho kilikuwa na wanachama watano lakini hadi kifikia sasa kituo hicho kina jumla ya wanachama hai 160 jambo ambalo amesema kuwa ni la kujivunia.
Amesema kuwa swala la kusimamia haki za binadamu sio jambo dogo kama watu wanavyolitamka midomoni bali kinachotakiwa ni kusimamia haki huku ukiishi ndani ya haki za binadamu na hapo ndipo utafanikiwa kutekeleza hilo.
Katika mkutano huo uliambatana na maonyesho mbalimbali ambayo yalikuwa na lengo la kuwaonyesha wanachama wake kutoka katika maeneo mbalimbali jinsi kituo hicho kinavyofanya kazi zake,na hapo chini nimekuwekea picha kadhaa za matukio mbalimbali katika kituo hicho
Wakuu wa idara mbalimbali za kituo hicho wakiendelea kutoa maelezo ya kina jinsi kituo hicho kinavyoendesha shughuli hizo hapa nchini. |
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa LHRC ndugu GEOFREY MMARI akizungumza na wanachama wa kitio hicho waliojitokeza katika mkutano huo unaoendelea katika makao makuu ya LHRC Jijini Dar es salaam. |
Waimbaji wa kwaya maarufu ya kituo hicho kwaya ya mwalusanya wakitoa burudani ya aina yake wakati wa shughuli hizo zikiendelea |
No comments:
Post a Comment