Kampuni ya mafuta na gesi ya Swala
(Tanzania) Plc ("swala" au "Kampuni") inayo furaha
kutangaza kwamba imefikia makubaliano ya kugawana umiliki na Kampuni ya Tata
Petrodyne Limited ("TPL"), kampuni ambayo ni sehemu ya Kampuni ya
Kimataifa ya Tata sons Limited, ambapo TPL itakuwa ikifanya shughuli zake
kwenye maeneo ya leseni ya Pangani na Kilosa-Kilombero nchini Tanzania.
Hii
itaiwezesha Kampuni ya swala kubaki kwenye maeneo yake ya leseni na ili kupata
fedha kwa ajili ya shughuli za utafutaji hapo baadaye katika njia ambayo
itapunguza hasara kwa wanahisa wake wa sasa.
Kampuni ya Tata Sons Limited ni
Mratibu wa uendeshaji wa shughuli kubwa za makampuni ya Tata na kumiliki hisa
zote muhimu kwenye makampuni haya, na kwa kawaida inajulikana kama kundi la
Tata (Tata Group). Kundi la Tata lina mtaji wa soko wa takribani dola za
Kimarekani bilioni 110 na inawakilisha zaidi ya asilimia 8 ya jumla ya mtaji wa
soko katika soko la hisa la Bombay.
Katika sekta ya mafuta na gesi, makubaliano ya
kugawiana umiliki ni makubaliano yaliyoingiwa kwa mmiliki wa leseni moja au
zaidi (anayegawa umiliki huo) na kampuni nyingine ambayo inataka kupata asilimia
ya umiliki wa leseni hiyo kwa ajili ya kutoa huduma (na 'kujimilikisha). Makubaliano
ya kugawana umiliki yanatofautiana na shughuli za kawaida kati ya wakodishaji
wawili wa mafuta na gesi, kwa sababu cha msingi kuzingatia ni utoaji wa huduma,
badala ya ubadilishaji rahisi wa fedha.
Makubaliano yaliyofikiwa na TPL:
·
Baada
ya kupokea vibali vya kiserikali kwa ajili ya uhamisho wa maslahi, kampuni ya
TPL itailipa kampuni ya swala Jumla ya
dola za kimarekani milioni 5.7 kwa ajili ya usawa wa maslahi, asilimia 25
katika leseni ya Kilosa-Kilombero na usawa wa maslahi wa asilimia 25 katika
leseni ya Pangani kama fidia zidi ya gharama zilizotumika zamani kwenye leseni;
·
Kampuni
ya TPL itaibeba Swala kwa gharama ya kisima cha awali kwenye leseni ya
Kilosa-Kilombero, hadi kiwango cha juu cha dola za kimarekani milioni 2.5
(swala inakadiria gharama za awali za kisima kuwa dola za kimarekani milioni
10.0);
·
Kampuni
ya TPL itaibeba Swala kwa gharama ya kisima cha awali kwenye
leseni ya Kilosa-Kilombero, hadi kiwango cha juu cha dola za kimarekani milioni
2.125 (swala inakadiria gharama za awali za kisima kuwa dola za kimarekani
milioni 8.5);
·
Kampuni
ya TPL itailipa swala zaidi ya dola za kimarekani milioni 1.0 dhidi ya gharama
ya kisima cha pili kufuatia ugunduzi wa kibiashara katika kisima cha awali
kwenye leseni ya Kilosa-Kilombero. Gharama zilizotumika zaidi ya kiasi hiki
zitabebwa na washirika kulingana na usawa wao.
·
Kwenye
ukamilisho wa Muamala uliotangazwa leo, usawa katika leseni mbili utakuwa:
|
Swala
|
TPL
|
* Otto
|
Kilosa-Kilombero
|
25%
|
25%
|
50%
|
Pangani
|
25%
|
25%
|
50%
|
* Otto Energy (Tanzania) Pty Ltd
“(Otto”) ni mmiliki mkubwa wa sehemu ya Otto Energy Ltd (ASX: OEL)
Kampuni inakadiria kuwa kwa sasa imejidhatiti
kikamilifu kwa majukumu yake yaliyobakia kwenye leseni zote mbili. Kampuni ya
swala ilishauriwa katika shughuli hii na kampuni ya First Energy Capital
("FIRSTENERGY") na kampuni ya TPL ilishauriwa na benki ya Rand
Merchant.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni
ya Swala Dk David Mestres Ridge alisema: "Kampuni inayo furaha kutangaza
makubaliano ya swala Tanzania na kampuni ya TPL inayofahamika kwa sifa nzuri.
Ugawaji huu wa umiliki utatoa mwanya kwa Kampuni kufadhili majukumu yake
iliyojiwekea kwa njia ambayo inapunguza hatari kwa wanahisa wetu bila kuwa na
haja ya kuongeza hisa ya ziada za kianzio kwa wakati huu.
Napenda kutoa shukurani kwa FirstEnergy
kwa ajili ya mbinu zao za kitaalamu katika kuendesha mchakato wa kugawa umiliki
na kwa ajili ya kuzalisha riba kutoka kwenye makundi hayo yanayoheshimika sana.
Kwa sasa kampuni ya Swala itazingatia
kupata ridhaa muhimu na vibali vya kiserikali ili kuruhusu ubia mpya
uliotengenezwa ili kuendeleza mipango ya uchimbaji kwenye leseni zote mbili na
tunataraji kuboresha soko pamoja na mwongozo wa lini mambo haya yaanze.
Kuhusu Swala:
Swala ni kampuni ya kwanza ya
mafuta na gesi kutajwa kwenye orodha ya soko la hisa la Afrika Mashariki. Ni
kampuni iliyo chini ya kivuli cha Swala Energy Limited, kampuni ambayo kwa upande wake iko kwenye orodha ya soko
la hisa la nchini Australia (ASX) na ikijulikana kwa kifupi kama
"SWE". Swala inamiliki mali katika nchi za Afrika Mashariki
zinazopitiwa na mfumo wa bonde la ufa na ina ardhi yenye eneo la zaidi ya
kilomita za mraba 17,500. Swala inafanya kazi kwa
juhudi na ina mpango wa maendeleo ya biashara ili kuendelea kukua hasa katika
majimbo
ya afrika Mashariki yenye nishati ya hydrocarbon.
No comments:
Post a Comment