Mkurugeni Mtendaji wa Taasisi ya REPOA Profesa SAMWELI WANGWE akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa siku mbili unaoendelea jijini Dar es salaam |
Wanawake
wafanyabiashara Masokoni na wajasiriamali nchini wametakiwa kungana na kuunda
umoja imara kwa lengo la kufikisha matatizo yao kwa pamoja kwa watunga sera na
serikali ili waweze kuchangia katika kukuza uchumi wa Taifa.
Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na
Mkurugeni Mtendaji wa Taasisi ya REPOA
Profesa SAMWELI WANGWE katika kongamano la siku mbili lililowakutanisha
wanawake wafanyabishara masokoni kutoka zaidi ya mikoa tisa nchini Tanzania
ambapo amesema kuwa ipo haja ya wanawake hao kuungana kwa pamoja kutetea haki
zao kwani ni ukweli usiopingika kuwa wanachangia kwa kiasi kikubwa sana katika
ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Wanawake mbalimbali ambao ni wafanya biashara katika masoko wakisikiliza kwa makini wakati mkutano huo ukiendelea mapema leo |
Amesema
kuwa wanawake wajasiriamali nchini ambao wanafanya biashara zao katika masoko
mbalimbali wamesahaulika sana na serikali na mamlaka husika jambo ambalo
limesababishwa na wanawake wenyewe kutokuwa na umoja ambao unaweza kutoa sauti
moja kwenda serikali kudai haki zao.
Anaongeza
kuwa kundi kubwa la wanawake ambao ni wajasiriamali nchini wamekuwa hawaguswi
moja kwa moja na ukuaji wa uchumi wa Taifa kwa kuwa wamekuwa hawashirikishwi
katika mambo ya msingi ambayo yatawasaidia kuinua uchumi na biashara zao
binafsi jambo ambalo linafanya uchumi wa Taifa kukua lakini haumgusi moja kwa
moja mwanamke huyo ambaye yupo katika biashara zake.
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la EQUALITY FOR GROWTH (EFG) akifanya mahojiano na wanahabari kuhusu lengo la kuandaa mafunzo hayo maalum kwa wanawake hao
|
Aidha
ameongeza kuwa tatizo lingine linalowakumba wakina mama hao ni kutokutengewa
mazingira mazuri na manispaa husika kwa ajili ya kufanyia biashara zao kama
ilivyo katika mataifa mengine jambo ambalo limekuwa likiwapatia usumbufu mkubwa
wakina mama hao katika harakati zao za kufanya biashara.
Akizufumza
na mtandao huu Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la EQUALITY FOR GROWTH
(EFG) ambao ndio waandaaji wa Kongamano hilo la siku mbili Bi JANE MAGIGITA
amesema kuwa kongamano hilo limeandaliwa mahususi kwa ajili ya wanawake hao
kuwasaidia kutambua majukumu yao na kuwaunganisha kwa pamoja kwa lengo kutambua
haki zao na mahali pa kuzipata.
Picha ya pamoja kwa washiriki wa mkutano huo |
Amesema
kuwa wanawake wanaofanya kazi katika masoko ya Tanzania wamekuwa wakikumbana na
matatizo mengi kama kukosa sehemu halali za kufanyia biashara,uonevu kutoka kwa
wanaume,uelewa mdogo wa sheria za biashara na elimu ya biashara jambo ambalo
amesema kuwa wanahitaji makongamano kama hayo ili yawasaidie katika kuzitambua
haki na shughuli zao.
No comments:
Post a Comment