Tuesday, July 28, 2015

CCM sio mama yangu,Mji wa Dodoma wasimama Kwa Muda Wakati Lowasa Akifanya Maamuzi Magumu

 Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akizungumza na mamia wakati wa kutangaza adhima yake ya kujiunga na Chadema katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya kujunga kwake katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akimpa kadi ya uanachama Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Regina Lowassa leo katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akimkabidhi kadi ya uanachama wa chama hicho,Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa leo katika hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Picha zaidi ingia MICHUZI BLOG



SHUGHULI zimesimama katika mji wa Dodoma kwa muda wote ambao Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeutumia kumtambulisha Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kujiunga na Chama hicho. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Mbali na kusimama kwa shughuli wananchi ambao walijaa katika kila kona ambapo kulikuwa na mgahawa au sehemu ya runinga walisikika kumuunga mkono huku wengine wakichana kadi za CCM.

Aidha, vikundi vikundi vya watu katika maeneo mbalimbali ambapo kulikuwa na runinga wakishangilia na kufurahia ambao umefanywa na Lowassa kwa kujiunga katika Chadema na kuendeleza mapambano na Ukawa.

Baada ya Lowassa kutangaza kuwa amejiunga rasmi na chama hicho makundi ya vijana pamoja na watu wazima walionesha kupiga kelele za shangwe huku wakisema mwisho wa CCM umefika.
Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Endtime Harvest na Katibu wa Umoja wa Madhehebu ya Kikristo mkoa wa Dodoma, Dk Elia Mauza akizungumza na Mwanahalisi Online amesema kitendo cha Lowassa kuhamia upinzania ni ujasiri wa hali ya juu na ni mpango wa Mungu.

Amesema kati ya viongozi walioonesha ujasiri ndani ya serikali ya CCM alikuwa ni Lowassa ambaye alikuwa mkweli na mbunifu katika kuhakikisha maisha ya watanzania wainuka kimapato.

Askofu Dk Mauza aliwataka watanzania wakumbuke kuwa mwenye maono ya kuazisha shule za kata alikuwa Lowassa lakini baada ya kufanyiwa fitina na kujiuzulu uwaziri mkuu kwa faida ya serikali hadi sasa shule hizo zimedorora .

Hata hivyo amesema kitendo cha uongozi wa Chadema kwa kushirikiana na Ukawa kumkaribisha kada hiyo kujiunga na wao ni dalili za ukomavu wa kisiasa ambazo zinalenga kuwapatia ukombozi watanzania wanyonge.

Kwa upande wao wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kwa Machinga waliliambia gazeti hili kuwa kuijiunga kwa Lowassa Ukawa ni dalili za ukombozi kwa watanzania wanyonge.

Mmoja wa wasomi wa Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM ambaye hakutaka jina lake litajwe aliliambia gazeti hili kuwa kitendo cha kuingia upinzani ni ishara tosha ya kuiondoa CCM madarakani.

“Hata huyu Dk .Magufuli ambaye anashangiliwa kuwa ni jembe hakuna jambo lolote ambalo anaweza kulifanya kuwa jipya ndani ya kutokana na mfumo ambao hupo kwa sasa mfumo wa CCM umejaa ufisadi na kulindana kwa wala rushwa

No comments: