Viongozi wa chama cha wananchi CUF wakiongiozwa na mama MAGDALENA SAKAYA ambaye ni naibu katibu mkuu wa chama hicho wakijitokeza mbele ya wanahabari leo |
Baada ya jana kuzagaa
habari mbalimbali zikielezea kuwa chama cha wananchi CUF kimejiondoa katika
ndoa ya muungano wa umoja wa katiba ya
wanahanchi UKAWA,viongozi wa chama hicho leo wameibuka na kutoa utetezi juu ya
swala hilo.SHUGHUDA WAKO EXAUD MTEI ANAELEZA ZAIDI----------
Katika hali isiyokuwa
ya kawaida jana katika mkutano wa umoja huo uliofanyika katika ukumbi mmoja jijini Dar es salaam ulishughudia
mkutano huo kuendelea huku kukiwa hakuna uwakilishi wa chama cha wananchi CUF
jambo ambalo lilizua mijadala kila kona kuwa umoja huo umevunjika rasmi na
chama hicho kimejiondoa katika ndoa hiyo.
Mapema leo jijini dare
s salaam katika mkutano uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama hicho
baina ya viongozi wa chama na wanahabari,Naibu katibu mkuu wa chama hicho mama
MAGDALENA SAKAYA amewaeleza wanahabari kuwa ni kweli kuwa chama chao hakikuweza
kushiriki katika mkutano wa jana kwa kile alichojitetea kuwa sababu za kikatiba
ndani ya chama hicho na kwa kuwa kuna maamuzi makubwa ya kinchi yanayoendelea
baina ya umoja huo wameona ni muda sasa wa kuita mkutano wa baraza kuu la chama
hicho kwa dharura kushauriana mambo kadhaa kabla ya kuuendelea na ndoa hiyo ya
vyama vinne.
“Baada ya kikao cha
ukawa cha terehe 11,mwezi wa saba viongozi wa chama chetu akiwemo mwenyekiti wa
chama,naibu katibu mkuu na wakurugenzi tumekuwa na vikao vyetu vya ndani kwa
lengo la kuweka mambo flani sawa kabla ya kuamua,na ndiyo maana jana hatukuweza
kuonekana katika mkutano huo”amesema SAKAYA
Amesema kuwa
kutokuhudhuria kwa kikao cha jana tarehe 14 kilichokuwa kinatajwa kuwa ndio
kitatoa mgombea wa umoja huo haina maana kuwa chama hicho kimesusia umoja huo
na kuongeza kuwa hawawezi kufanya hivyo kwa kuwa hata jina na maana ya umoja
huo umeasisiwa na kiongozi wa chama hicho profesa lipumba.
Chama hicho kimeamua
kuita mkutano wa baraza kuu wa dharura terehe 25 mwezi huu kujadiliana maswala
maalum likiwemo la ushiriki wao ndani ya ukawa na baada ya hapo ndiyo watajua
kama wanaendelea na ndoa hiyo ama imekufa
Katika hali ambayo
imezua maswali mengi naye Mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama hicho bwana ABDUL KAMBAYA amesema kuwa
viongozi wa chama hicho akiwemo mweyekiti wa chama hicho hawakuwa na taarifa
yoyote ya mkutano wa ukawa jana tarehe 14 huku akisema kuwa mwenyekiti wa chama hicho
alipokea ujumbe wa kualikwa katika mkutano huo jana saa tatu jambo ambalo
lilimwia ngumu yeye kuamua kufika kwake.
“Ni kweli kuwa kikao
cha mwisho cha ukawa kilitangaza kuwa tarehe 14 ndiyo tutamtoa mwali wetu wa
urais na mh LIPUMBA alikuwepo,lakini katibu wetu wa ukawa ambaye ni DK SLAA
ndiye mwenye jukumu la kutoa taarifa kwa chama kuwa mkutano huo ni wapi
unafanyika mapema ili kiongozi wetu aweze kufika lakiini taarifa haikutufikia
kwa wakati na ndio sababu nyingine ya sisi kushindwa kufika jana”Ameeleza
kambaya.
Aidha kambaya amesema
kuwa sababu nyingine iliyowafanya viongozi wa CUF kujitoa kwanza katika
mchakato huo ni kile kinachoitwa kudharaulika kwa mwenyekiti wao,amesema kuwa
ilikubalika kuwa tarehe 14 ndiyo angetangazwa mgombea wa ukawa lakini cha
kusikitisha sana terehe 12 tayari kuna vyombo vya habari vilikuwa vinamtangaza
mgombea wa umoja huo na vyombo vingine vya habari vikienda mbali hadi kutaja
kura aliopata katika mchakato huo.
Amesema kuwa hali hiyo
imeamsha jazba na hasira baina ya viongozi na wanachama wa chama hicho chenye
maskani yake buguruni Dar es salaam na kuamua kusitisha kwanza ushiriki wao
katika mchakato huo na kurudi kwa wanachama na viongozi kuchukua ushauri wao
kabla ya kuamua jambo la kufanya.
Akizngumzia kile
ambacho kilizngumzwa jana mna mwenyekiti mwenza wa mkawa JAMES MBATIA kuwa
umo9ja huo tayari wameshampata mgombea wa uraisi na muda wowote watamtaja
--------amesema kuwa swala la urais ndani ya ukawa sio jambo kubwa sana kwa
kuwa sifa za mgombea wanayemtaka wameshaziweka wazi hivyo ni kama
ameshapatikana ila swala kubwa ni maridhiano na umoja ndani ya umoja huo
No comments:
Post a Comment