HAMAD RASHID akisalimiana na wanachama wa chama cha Alliance for Democtratic Change (ADC) wakati akiwasili katika mkutano huo |
Aliyekuwa mbunge wa
jimbo la wawi Zanzibar kupitia chama cha wananchi CUF ambaye hivi majuzi
ametangaza kukiahama chama hicho na kujiunga na chama kipya cha ADC Mh HAMAD
RASHID ameitaka Tume ya Taifa ya uchaguzi kufanya kila njia kuhakikisha kuwa watanzania
wote wenye sifa za kupiga kura wanajiandikisha ili waweze kutimiza haki yao
hiyo ya msingi.EXAUD MTEI anasimulia----
Wanachama wa Alliance for Democtratic Change (ADC) wakiwa katika mkutano huo |
Kauli hiyo imekuja
wakati zoezi la uandikishwaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura likiwa
linaendelea katika mkoa wa Dar es salaam ambapo limezua gumzo kubwa kutokana
na kasoro mbalimbali ambazo zinaonekana kujitokeza katika zoezi hilo jambo
ambalo linalalamikiwa na wadau wa maswala ya siasa kuwa linaweza kuwanyima
watanzania wengi haki yao ya msingi ya kupiga kura.
Hamad Rashid ametoa
kauli hiyo mapema leo wakati wa zoezi la uchukuaji wa form za kuomba ridhaa ya chama
hicho kipya ya kuwania nafasi ya urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ambapo
wanachama mbalimbali wamejitokeza kuiwania nafasi hiyo.
Mh Hamad amesema kuwa
haki ya kuchagua na kuchaguliwa ni haki ya kila mtanzania mwenye kutimiza
vigezo hivyo lazima tume ifanye kila njia kuhakikisha kuwa hakuna mtanzania
anayeachwa nyuma kutokana nna sababu yoyote kwani kama watanzania watakosa haki
ya kupiga kura watakuwa wamekosa haki ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Aanayekabudhiwa form hapa ni aliyewahi kuwa mgombea wa kiti cha uenyekiti wa chama cha wananchi CUFChifu Yemba naye anaomba nafasi ya kugombea urais wa Tanzania |
Aidha akizngumza na
wagombea mbalimbali waliojitokeza kuchukua form pamoja na wanachama wa chama
hicho ambacho kinajinasibu kuwasaidia watanzania hasa wa hali ya chini amesema
kuwa ni muda wa watanzania kuchagua viongozi bila kujali aina au maumbili ya
mgombea kwani hata walemavu wana haki ya kuchagua na kuchaguliwa hivyo chama
cha ADC kimekuwa kikiwapa watanzania wote nafasi bila kujali mapungufu yao.
Katika hatua nyingine
mtandao huu umedokezwa kuwa mh Hamad Rashid anataraji kuchukua form ya kuomba
ridhaa ya chama hicho kuwania nafasi ya urais huko Zanzibar.
No comments:
Post a Comment