Ikiwa imesalia miezi
kadhaa kwa Tanzania kuingia katika zoezi
kubwa la uchaguzi mkuu,viongozi na wale wote wanaowania nafasi za uongozi
wametakiwa kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unakuwa ni chanzo cha kukuza umoja na
amani iliyopo Tanzania bila kusababisha aina yoyote ya vurugu ambazo zinaweza
kuwagharimu watanzania.
Kauli hyiyo imetolewa
leo jijini Dar es salaam na kiongozi mkuu wa mashia Tanzania sheikh HEMED
JALALA katika muendelezo wa maadhimisho ya siku ya QUDS siku ambayo huazimishwa
kila inapofika ijumaa ya mwisho kabla ya sikukuu ya IDD,siku ambayo waislam hao
wameitumia kuhamasisha amani katika mataifa yanayokosa amani hiyo likiwemo
taifa la palestina.
Akizungumza na
wanahabari sheikh JALALA amesema kuwa amani katika taifa lolote ndio kiini cha
maendeleo huku akisema kuwa viongozi wakubwa wa Africa kama mwalimu nyerere na nelson
Mandela walifakiwa kukuza amani na kuisisitiza sana barani Africa hivyo ni
jukumu la viongiozi wetu kuienzi amani iliyopo
Amesema kuwa siku ya
QUDS ni siku ya kuwakumbuka wanyonge na wale wote ambao wanakumbana na dhuluma
za aina mbalimbali hivyo wametumia siku hiyo kulikumbuka taifa la palestina
likiwa ni taifa ambalo watu wake wamekuwa wakikumbana na adha hiyo ya kuonewa
na kudhulumiwa ardhi yao taktribani miaka 67 sasa.
Ameongeza kuwa waadhrika wakubwa katika nchi ambayo
amani imekosekana kama palestina ni wazee,wakina mama,pamoja na watoto bila
kujali dini zao wala kabila hivyo ni lazima dunia kwa umoja wetu tuamke na
kuwatetea wananchi wa taifa la palestina ambao wanakumbana na mateso ya aina
hiyo.
Amesema kuwa
kiinachotokea nchini Palestina kinaweza kutokea katika taifa lolote hata Tanzania
hivyo ni lazima kwa pamoja tuungane kuilinda na kuitetea amani tuliyonayo.
No comments:
Post a Comment