Moja kati ya matukio ya kujichukulia sheria mkononi yaliyowahi kutokea nchini. |
Kituo cha sheria na haki za binadamu Tanzania LHRC leo wametoa Report ya Haki za binadamu kwa kipindi cha nusu mwaka huu wa 2015 report ambayo inaonyesha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika Nyanja mbalimbali.
Taarifa hiyo ambayo ni matokeo ya Tafiti mbalimbali zilizofanywa na kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC inaonyesha kuwa swala la haki ya kuishi kwa watanzania bado imeendelea kukiukwa ambapo katika utafiti huo unaonyesha kuwa kwa kipindi cha nusu mwaka pekee watu takribani 366 waliuawa kutokana na raia kujichukulia sheria mkononi jambo ambalo limetajwa kuangamiza maisha ya watanzania walio wengi.
Mtafiti kutoka kituo hicho ndugu PAUL MIKONGOTI akizngumza na wanahabari wakati akitoa ufafanuzi wa Report hiyo leo Jijini Dar es salaam |
Akitoa ufafanuzi juu ya Report hiyo mtafiti kutoka kituo hicho ndugu PAUL MIKONGOTI amesema kuwa matatizo ya kujichukulia sheria mkononi yamekuwa yakiwahusisha zaidi watu wanaokuwa na tuhuma za wizi,na hasa vibaka,huku akisema kuwa matukio mengi ya kujichukulia sheria mikononi yamekuwa hayatolewi taarifa kwenye vyombo vya habari hasa matukio yanayotokea vijijini.
Mauaji mengine ambayo yamejitokeza katika report hiyo ni mauaji ya askari hasa wawapo kazini,ambapo kwa kipindi hiki cha nusu mwaka vituo vinne vilivamiwa na kusababisha vifo vya askari watatu jambo ambalo limeendelea kugarimu maisha ya askari hao.
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za Binadamu LHRC Bi HELLEN KIJO BISIMBA akifafanua jambo |
Tofauti na haki ya kuisha ambayo imejitokezaa katika Report hiyo iliyotolewa leo haki nyingine ambazo zimeonekana kukiukwa kwa hali ya juu ni pamoja na haki za wanawake na watoto,haki ya bkiupata habari na uhuru wa habari,haki ya afya bora,haki ya kupiga kura,pamoja na maswala ya rushwa na utawala bora yamejitokeza sana katika report hiyo.
Akizungumzia Report hiyo mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC Bi HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa swala la kujichukulia sheria mkononi limezidi kuwa kubwa na imefika kipindi sasa kwa watuhumiwa wa kuchukua sheria mkononi na wale wa mauaji yatokanayo na imani za kishirikina washughulikiwe kama wahalifu wengine kwa mujibu wa sheria za nchi jambo ambalo linaweza nkupunguza hali hiyo
Aidha ameishauri serikali kuhakikisha kuwa inarekebisha mfumo wa utoaji wa haki unaboreshwa ili kutopa haki kwa wote huku ikiendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kurekebisha mkifumo hiyo.
Taarifa iliyotolewa leo imejikita zaidi katika maeneo machache ya haki za binadamu ambayo yameoinyesha kuwa na ukiukwaji wa hali ya juu katika kipindi cha nusu mwaka ambapo taarifa kamili ya hali ya haki za binadamu nchini itaandaliwa mwishoni mwa mwaka.
UKITAKA KUSOMA TAMKO NZIMA LIPO CHINI HAPO
No comments:
Post a Comment