Katibu mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine (wa pili) akifungua semina ya makatibu wakuu wa vyama vya mpira wa miguu nchini kuelekea kwenye michuano ya airtel.JPG |
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Mwesigwa Selestine leo amefungua
semina ya makatibu wakuu wa vyama vya soka vya mikoa nchini (FA's) kuhusu maandalizi ya michuano ya airtel.
Katika ufunguzi wa semina hiyo, Mwesigwa amewaomba viongozi hao kuzingatia kanuuni na mahitaji katika michuano ya Airtel inayoshirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 17 ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni.
Mwesigwa amesema viongozi hao wakichagua vijana wenye umri sahihi wa kushiriki kwenye michuano hiyo itatoa fursa kwa makocha kuchagua wachezaji wenye umri halisi kwa ajili ya maendeleo ya mpira wa nchi yetu.
Aidha Mwesigwa ameipongeza kampuni ya simu za mkonono ya Airtel kwa kuendesha michuano hiyo kila mwaka, ambapo kwa sasa vijana watatu wapo katika kituo cha mpira miguu kilichopo Dakar - Senegal wanaposoma masomo ya kawaida na kufundishwa mpira wa miguu, huku wakitafutiwa timu za kucheza nje ya Afrika na kufanya majaribio sehemu mbalimbali Ulaya.
No comments:
Post a Comment