Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akizngumza katika semina hiyo leo jijini Dar es salaam |
Sheikh
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema kuwa
jukumu la kuwasaidia watu wanaodhulumiwa na kuonewa katika mataifa mbalimbali
hususani taifa la palestina ni jukumu la watu wa aina zote bila kujali
dini,utaifa wala utofauti wowote uliopo.
Kauli hiyo ameitoa leo
jijini Dar es salaam katika semina maalum iliyoandaliwa na waislam wa dhehebu
la shia kwa waialam pamoja na watu wote wanaopinga dhuluma na uonevu mbalimbali
duniani,semina iliyofanyika jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na waumini wa
dini ya kiislam pamoja na dini zote na wapinga uonevu wote.
Baadhi ya waumini waliohudhuria semina hiyo |
Semina hiyo ni
mwendelezo wa maadhimisho ya siku ya QUDS duniani siku ambayo ni maalum kwa
watu wanaopinga dhuluma na kuthamini haki za binadamu ambapo katika maadhimisho
hayo waumini hayo wameyatumia kutafakari na kukemea kwa pamoja kile ambacho
kinaendelea katika taifa la palestina.
Baadhi ya picha ambazo zinaonyesha madhara ya vita inayoendelea nchini palestina |
Akizungumza katika
semina hiyo mgeni rasmi ambaye ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Alhad Mussa Salum amesema kuwa siku
ya QUDS ni siku ya watu wote na madhehebu na dini zote na sio siku ya
wapalestina pekee kwa sababu ni siku ambayo inatumika kupinga kwa sauti moja
uonevu wowote ambao unaendelea katika mataifa mbalimbali duniani.
Amesema kuwa sisi kama
Taifa la Tanzania ni siku muhimu ya kutafakari amani ya dunia ikiwa ni pamoja
na kupinga kwa sauti moja dhuluma yoyote inayoendelea dhidi ya watu wa
palestina na mataifa mengine duniani.
Waumini hao wameanza
kuadhimisha siku hiyo jana ambapo walifanya matembezi ya amani katika jiji La
Dar es salaam kuwakumbusha watanzania juu ya kuiombea na kuisaidia nchi ya
pelestina kutoka katika machafuko ambayo yanazidi kugharimu maisha ya watu
No comments:
Post a Comment