Thursday, July 9, 2015

UHAMIAJI--AWAMU YA NNE TUMEKUWA BORA SANA

Kamishina wa Fedha na Utawala wa Idara ya Uhamiaji,
 Piniel Mgonja akizungumza na waandishi habari juu
 ya mafanikio ya idara ya uhamiaji
katika awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete
 iliyofanyika leo Makao Makuu ya
Idara hiyo Kurasini jijini Dar es Salaam.


IDARA ya Uhamiaji katika awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete imeingiza zaidi ya Sh.bilioni 474 kwa kipindi cha miaka 10 ambayo imetokana na maboresho mbalimbali katika idara hiyo.
           Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamishina wa Fedha na Utawala,Piniel Mgonja amesema kuwa katika awamu ya nne uhamiaji imeweza kufanya kazi ya kisasa kutokana na mifumo pamoja na ujenzi wa Chuocha kuendeleza maafisa wa idara hiyo.
            Amesema katika utoaji wa hati ya kusafiria kwa mwezi wanatoa hati 5000 tofauti na miaka 10 iliyopita ambapo walikuwa wakitoa hati 2500 ambayo ilikuwa ikitokana na kuchukua muda mrefu wa kuchapa kuliko ivyo sasa zinachapwa kwa kompyuta.
         Mgonja amesema katika suala la uhamiaji bado changamoto kutokana na kuwa na uwazi katika mipaka ambapo walifanya uparesheni kuwakamata zaidi ya watu 74 000 kati ya hao watu zaidi 66000 waliondolewa nchini.
         Amesema wamezidi kuimarisha katika udhibiti wa njia za mipaka ili nchi isiweze kugubikwa na wahamiaji haramu.

            Amesema katika kipindi kijacho hati kusafiria kwa nchi za Afrika Mashariki itakuwa moja ya kimataifa ili kuondoa usumbufu kwa wateja wao kutafuta mara kwa mara kwa hati ya kusafiria kwa Afrika Mashariki

No comments: