MBUNGE wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu, amesema chama chao kinatarajia kupata wanachama wengi baada Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kujiunga na chama hicho.
Lissu ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo taarifa kwamba wapo wanachama wa Chadema ambao watakihama chama hicho kutokana na kutokubaliana na ujio wa Lowassa ndani ya Chadema.
Akizungumza leo na waandishi wa habari Lissu amesema, “Kama wapo watakao jiondoa Chadema, wengi zaidi watakuja. Tupo katika kipindi ambacho hatujawahi kuwepo tangu mfumo wa vyama vingi uanze.
Mfumo tawala unabomoka vipande vipande. Unapo bomoka, dalili zake ni watu ambao wamekuwa katika mfumo huo kuondoka kama alivyofanya Lowassa.”
“Mabadiliko katika nchi yanatokea pale mfumo tawala unapo pasuka. Lowassa ni mfano mzuri.
Tunamkaribisha kwetu sio kwa sababu ni mwanasiasa msafi. Tumempokea kwa sababu tunaongeza nguvu kubwa kwa wale wanaotaka mabadiliko. Imetokea Zambia Mawawi, Nigeria na Kenya,” amesema Lissu.
Akizungumza kuhusu Chadema kumtuhumu Lowassa kwamba “ni fisadi” kabla ya kujiunga na chama hicho Lissu amesema, “…hatukuwa na makosa hata kido kumweka Lowassa katika kundi la watuhumiwa wa Richmond. Mambo yalizungumzwa bungeni. Aliwajibika na amesema mwenyewe aliwajibika.”
“Alijiuzuru uwaziri mkuu kwa sababu ya Richmond. Tulimweka katika orodha ya mafisadi kwa sababu ya Richmond. Na jana alisema alimwambia rais “tuvunje mkataba” rais akaataa. Angefanyeje?. hilo ni vumbi, litakapo tulia Chama Cha Mapinduzi na mfumo tawala utakuwa umeanguka, tutajenga nchini.Bila kuvunja mfumo tawala hakuna kusonga mbele,” ameeleza Lissu.
No comments:
Post a Comment