![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdVeXN8_b29f5Wekx7wK6v0XVI1bErPQ09rTgP5FU-vGp3yqbr4hPSTY31XsQdtpcwZa1RxmoNa6VFEPuIXqNl9aEJdvRf1OFvuytjD_HhhStOeY3e50GEV1GMxFTZaJREeHnUCziUnw/s400/tigopesa.jpg)
Lengo letu ni kuhakikisha kuwa wadau
wote wa Tigo Pesa, ambao ni pamoja na wateja binafsi, mawakala wa reja reja na
washirika wetu wa kibiashara ambao watashiriki kwenye gawio la faida hii ni
kutokana na thamani ya kietronikia (e-value) ambayo wamehifadhi kwenye pochi
zao za Tigo Pesa," alisema Mkuu wa Huduma za kifedha wa Tigo, Ruan
Swanepoel.
Hii ni faida ya pili ya hisa kwa mwaka
2015 ambayo pia ni ya tano tangu Tigo ilipoanza kugawa faida inayotokana na akaunti
za Tigo Pesa zinazoratibiwa na benki kubwa nchini Tanzania, kwa kweli
tunafuraha kutangaza mgawanyo huu kwa watumiaji wetu waaminifu wa Tigo Pesa.
Malipo haya yanaonyesha dhamira yetu ya kutoa huduma za kifedha kwa wateja wetu
nchi nzima kwa ujumla, "alisema Swanepoel.
Tigo ni kampuni ya mawasiliano ya simu ya kwanza na pekee
duniani hadi sasa kushirikisha faida zake zitokanazo na akaunti ya fedha ya
simu za mkononi, katika mfumo wa ugawaji kwa kila robo mwaka, aliongeza.
Tunaamini
ugawaji huu wa faida ya hisa ya Tigo Pesa katika mwaka 2015 utaleta unafuu kwa
mamilioni ya watumiaji wa Tigo Pesa katika kufanikisha mipango yao ya kifedha.
Mawakala wa Tigo Pesa wameona baadhi ya faida kubwa inayotokana na mpango huu
kama wanavyoshuhudia ukuaji wa biashara zao. Haya ni matokeo ya kuongezeka kwa
wateja na kushiriki faida, "alisema.
Swanepoel aliongeza kwa kusema kwamba, kabla
ya faida kwa wateja huwa inakokotolewa kwa kuzingatia wastani wa salio la kila
siku lililohifadhiwa kwenye pochi zao za Tigo Pesa. Malipo ya kiasi cha bilioni
3.314 yanakaribiana na yale ambayo kampuni ililipa katika robo mwaka ya kwanza
ya mwaka 2015.
Mpango huu wa mgawanyo wa faida za hisa za Tigo Pesa ni
kwa mujibu wa waraka wa Benki Kuu uliotolewa mwezi Februari 2014. Hadi sasa
kampuni imelipa jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 27.2 kwa watumiaji wa Tigo Pesa katika robo tano
za mwaka za malipo tangu kuanzishwa kwa huduma hii mwezi Julai 2014 .
No comments:
Post a Comment