Mastaa wa Bongo,Wema Sepetu,Steve Nyerere na mwimbaji wa taarab kutoka kundi la Jahazi,Mzee Yusuf kwa nyakati tofauti wamechukua fomu za kugombea ubunge kupitia chama cha Mapinduzi(CCM).
Wema akiwa na wapambe wake wameelekea mkoani Singida ambapo amechukua fomu kugombea ubunge kwenye jimbo hilo kupitia viti maalum.
Steve Nyerere yeye amechukua fomu mapema leo kwenye ofisi za CCM,Kinondoni Kata ya Mkwajuni akigombea jimbo hilo la Kinondoni.
Mzee Yussuf amechukua fomu kugombea ubunge jimbo la Fuoni visiwani Zanzibar.
Wapambe wa Steve Nyerere wasanii wa Bongo Movie
No comments:
Post a Comment