Yale yaliyokuwa
yanasemwa kuwa Mbunge wa Monduli ED WARD LOWASA atajiunga na umoja wa katiba ya
wananchi ukawa sasa imekuwa rasmi baada ya umoja huo kujitokeza muda huu na
kumkaribisha rasmi na kusema kuwa sasa anakaribishwa yeye pamoja na watanzania
wengine kuwa wanakaribishwa kujiunga na harakati hizo.
Katika mkutano wa
wanahabari uliomalizika muda huu hapa makao makuu ya chama cha wananchi CUF
mkutano ambao umehudhuriwa na wenyeviti wote wa vyama hivyo wamesema kuwa sasa
rasmi wanamkaribisha lowasa kujiunga na harakati zao kwani bado wanaamini ni
mtu safi ambaye alichafuliwa na watanzania bado wanaimani nao japo kuwa
alitemwa katika mchakato wa chama cha mapinduzi.
Nje ya makao makuu CUF muda huu |
Mh mbatia anasema kuwa
umoja huo lengo lake ni kuondoa mfumo uliopo ambao unaongozwa na CCM hivyo
wwatafanya kila njia ambayo itasaidia kufanikisha zoezi hilo.
Maswali mengi ya
wanahabari yalikuwa yakiwataka viongozi hao kuonyesha kuwa LOWASA sio fisadi
kama ambavyo waliwahi kumshambulia viongozi hao wamesema kuwa kiongozi huyo sio
fisadi kwani hadi sasa hana kesi yoyote mahakani ya ufisadi.
Kuhusu mgombea wa urais
wa umoja huo mbatia anasema kuwa
mwanzoni mwa mwezi wa nane huku mwenyekiti wa chama cha NLD anasema kuwa
hakuna ubaya kama wakimchagua mh LOWASA kugombea nafasi hiyo.
Mkutano umemalizika kwa
viongozi hao kusema kuwa UKAWA iko imara na ndio tumaini jipya la watanzania na
hakuna mtu wa kuivuruga.
No comments:
Post a Comment