Kaimu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mama SOPHIA MJEMA akikabidhi kombe kwa kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo Jijini Dar es salaam mapema leo |
Jeshi la polisi kanda
maalum ya Dar es salaam leo limezindua rasmi mashindano ya michezo mbalimbali
yatakayoendeshwa jijini Dar es salaam ambayo yatashirikisha michezo yote,michezo
ambayo inalengo la kuwashirikisha wananchi wa rika na itikadi mbalimbali
mashindano yaliyopewa jina la KAMISHNA KOVA CUP.
Akifungua mashindano
hayo mkuu wa wilaya ya temeke ambaye kwa sasa ni kaimu mkuu wa mkoa wa Dar es
salaam mama SOPHIA MJEMA amesema kuwa mashindano hayo yamekuja kipindi kizuri
ambacho Tanzania inajiandaa na uchaguzi mkuu ambapo amesema kuwa ni vyema
mashindano hayo yatumike kuwaunganisha vijana na kuilinda amani na upendo
uliopo Tanzania.
Kukata utepe |
Mama Sophia amesema
kuwa kipindi cha uchaguzi ni nkipindi ambacho vijana ambao hawana shughuli
maalum wamekuwa wakirubuniwa na watu ambao hawaitakii mema Tanzania kwa kuwapa
hela ili wafanye lolota ili kuivuruga amani ya nchi jambo ambalo amesema
mashindano hayo yamekuja kuhakikisha kuwa vijana wanashitriki na kuacha kukaa
bila kitu cha kufanya na kuwafanya kujiepusha na makundi ya uvunjifu wa amani.
Naye mhasisi wa
mashindano hayo ambaye ni kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam ASP
SULEMAN KOVA amesema kuwa kupotia mashindano hayo jamii itafaidika kupata elimu
wa aina mbalimbali kama vile ujambazi,matumizi ya aina mbalimbali ya madawa ya
kulevya,wizi katika mitandao,uzururaji,na kukaa katika vijiwe bila kazi.Pamoja
na kujenga na kuimarisha ushirikiano baina ya jamii na jeshi la polisi.
Katika mashindano hayo
ambayo yanataraji kumalizika mwezi wa 11 baadhi ya zawadi kwa washindi ni
pamoja na vikombe,vyeti vya ushiriki na Fedha Taslim.
Wadau mbalimbali ambao wanashiriki katika mashindano hayo yaliyozinduliwa Jijini Dar es salaam |
No comments:
Post a Comment