Meneja wa Vifaa vya Huawei, Peter Zhang Nchini (kulia), akionesha aina ya simu ya Huawei Y 360 na Y 625 ambazo zina uwezo wa hali ya juu katika matumizi ya nyanja mbalimbali wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi katika uzinduzi wa simu hizo. Kushoto ni Meneja wa Vifaa na Intaneti kutoka Tigo, Mkumbo Myonga.
Meneja wa Vifaa na Intaneti kutoka Tigo, Mkumbo Myonga, akizungumza katika mkutano huo.
|
Wanahabri kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa ya uzinduzi huo.
Kampuni ya Tigo Tanzania
na kampuni ya kutengeneza simu za mkononi ya Huawei washirikiana kuzindua simu
mbili za kisasa, Huawei Y360 na Y625 ikiwa
mwendelezo wa ugunduzi na matumizi katika nyanja ya utandawazi.
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa simu hizo, Meneja wa vifaa vya Huawei, Peter Zhang,
amesema kuwa simu za Huawei Y360 na Y625 zina uwezo wa hali ya juu na
zinapatikana kwa bei nafuu
itakayozifanya zipate umaarufu sokoni.
“Tunafuraha ya kushirikiana na
kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania kwa mara nyingine tena tukiamini
kuwa uzinduzi huu wa simu za kisasa utaleta mafanikio na mabadiliko makubwa na
ya kisasa katika mawasiliano ,” Alisema Zhang.
“Simu ya Huawei Y360 inapatikana
kwa bei nafuu sana ikiwa katika mfumo wa android na kioo cha mbele chenye inchi
nne na kuipa sifa kubwa ya matumizi katika mitandao ya kijamii kama vile ‘Facebook’,
‘Instagram’, ‘Twitter’ na ‘WhatsApp’, na halikadhalika, simu ya Huawei Y625 ina
kioo cha mbele chenye ukubwa wa inchi tano, na uwezo wa kutumia laini mbili za
simu na ikiwa katika mfumo wa android,” aliendelea kusema.
Akizungumza kwenye
hafla hiyo, Mkuu wa kitengo cha vifaa na intaneti wa Tigo, David
Zacharia alisema kuwa, kampuni ya Tigo Tanzania imejitolea katika kuendeleza na
kubadilisha maisha ya Watanzania kuwa ya kidigitali, na uzinduzi wa simu mpya za
kisasa utaiwezesha jamii kukabiliana na hali ya kiteknolojia inayokuwa kwa kasi
na kuufanya ulimwengu wa mawasiliano kuwa kijiji kimoja.
“Simu Ya Huawei Y360 ni bora na inapatikana kwa bei nafuu
katika soko la ushindani ikiwa na uwezo wa kupiga picha kwa kutumia kamera zake
za mbele na nyuma na pia ina uwezo wa
kutumia laini mbili za simu kutoka mitandao tofauti huku ile ya Huawei Y625 ikiwa
na ubora wa kipekee na kioo cha mbele
chenye ukubwa wa inchi tano.” Alisema Zacharia.
Simu hizi zitapatikana katika maduka ya Tigo kwa bei nafuu,
ambapo Huawei Y360 itauzwa kwa Tsh. 160,000
na Huawei Y625 ikiuzwa kwa Tsh. 295,000.
Wateja watafurahia ofa kabambe kama vile kifurushi cha muda wa maongezi cha Tsh
5,000, data/intaneti ya 2GB na muziki bure kwa muda wa miezi sita.
|
No comments:
Post a Comment