Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Makambako, waliofurika kwa wingi wenye Polisi Makambako, Mkoani Mkoani Njombe leo Agosti 31, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake. Katika hotuba yake, Mh. Lowassa amewatoa hofu wana CCM wanaotaka kujiunga na Ukawa kutoogopa kuchukua uamuzi huo kwani huu ni mwaka wa mabadiliko. Pia amewaomba Watanzania wanaomuunga mkono katika mikutano yake ya hadhara kutoishia hapo na badala yake kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi wa Mwaka huu wa Oktoba 25 mwaka huu.
|
No comments:
Post a Comment