Friday, August 14, 2015

Soma hoja za MTATIRO kuhusu usafi au uchafu wa lowasa


Na. Julius Mtatiro -

(TAHADHARI: Kama una Jazba usichangie POST hii - Utakufa kwa Presha Bure, Posti hii inaweza kuibua hisia kali, hofu, wasiwasi na majuto ikiwa unakubaliana na maoni haya au unayapinga na ikiwa mgombea wako amegongwa mahali hapa au ameparazwa, jadili hoja wala usimguse mtoa hoja)
                                        Ndugu zangu, 
Jana Chama Cha Mapinduzi kimetoa orodha ya wagombea wake nchi nzima. Katika orodha hiyo kuna watuhumiwa wengi tu wa masuala ya ufisadi, kuna watuhumiwa wengi wa rushwa na wengine walikamatwa na kuhojiwa na TAKUKURU, kwa kifupi kuna watuhumiwa kibao sana.
Lakini kubwa kuliko yote USHAHIDI WA WAZI unaonesha kuwa hakuna mgombea hata mmoja wa CCM anaweza kupita kwenye kura ya maoni nchi nzima bila kutoa rushwa kubwa na ndogo, kwa wapiga kura wa kawaida na kwa viongozi wanaosimamia uchaguzi. Nina marafiki zangu wengi tu wameshinda na kushindwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM, kila mmoja (aliyeshinda na aliyeshindwa) wanasema kuwa PESA ndiyo inaamua nani hasa apitishwe ndani ya CCM.
Leo nataka kumuuliza ndugu yangu Humphrey Polepole na aje hapa anijibu kwa hoja. Je, msimamo na mtizamo wake juu ya rushwa ndani ya CCM uko namna gani? Nilipofuatilia mjadala kati yake na Mchungaji Msigwa nilimuona Polepole akisisitiza kuwa kiongozi akishatuhumiwa tu anapoteza political legitimacy ya kuwa kiongozi kwa sababu anakuwa amepoteza "moral authority" (mamlaka ya kimaadili).
Polepole amesisistiza kuwa Lowassa ni mtuhumiwa mkubwa wa ufisadi hasa kwenye eneo la RICHMOND na kwamba hawezi kumuunga mkono, katika hilo nakubaliana naye. Lakini pia nilitaraji Polepole atueleze kuwa Magufuli pia ni mtuhumiwa mkubwa wa ufisadi na hasa akihusishwa na uuzaji holela wa nyumba za serikali kwa manufaa binafsi na kuwapatia ndugu zake nyumba nyingine zenye thamani kubwa.
Kama kutuhumiwa tu kwa masuala ya kuvunja maadili kunamfanya mtu anyimwe haki ya kuwa kiongozi basi mwaka huu tumeingizwa chaka na CCM na UKAWA! Kwamba vyama vyote vimesimamisha wagombea ambao ni watuhumiwa wa ufisadi lakini hakuna mmoja kati yao aliyewahi kuthibitishwa kwamba amekula pesa ngapi kwenye ufisadi huo.
Polepole alikwenda mbali zaidi na kutoa sharti kubwa kwa uongozi wa juu wa CCM, kwamba uongozi huo ukate wabunge wote ambao wana tuhuma au wamepita kwa njia ya rushwa. Kwa bahati mbaya sana watuhumiwa wote wa ufisadi na rushwa ndani ya CCM wamerejeshwa kugombea ubunge na nyadhifa zingine, kina Andrew Chenge a.k.a Vijisenti, kina Prof. Tibaijuka a.k.a Hela ya Mboga n.k. Kuna watuhumiwa wengine wa utoaji rushwa wakati wa kura za maoni za CCM ambao walikamatwa na TAKUKURU na kuhojiwa, wote hawa wameshapoteza MORAL AUTHORITY na POLITICAL LEGITIMACY!
Polepole njoo usaidie kueleza watanzania nini ni mtizamo wako juu ya uchaguzi huu ambao CCM imesimamisha mgombea urais ambaye ni mtuhumiwa namba moja wa ufisadi wa UUZAJI WA NYUMBA ZA SERIKALI na UKAWA imemsimamisha mgombea ambaye ni mtuhumiwa wa ufisadi wa RICHMOND. Njoo utueleze msimamo wako juu ya uchaguzi ambao CCM imesimamisha zaidi ya robo tatu ya wabunge ambao ni watuhumiwa wa ufisadi mkubwa na utoaji rushwa wa wazi kwenye kura ya maoni dhidi ya UKAWA ambayo imesimamisha takribani zaidi ya ROBO TATU ya wabunge ambao hawajawahi kujihusisha na ufisadi wala kutoa rushwa kwenye kura za maoni za ndani ya vyama.
Na mwisho njoo utueleze tatizo la Rushwa na Ufisadi ni la kimfumo zaidi au ni la mtu? Njoo utueleze kuwa ni nani yuko kwenye nafasi nzuri ya kupambana na ufisadi, Magufuli ambaye yumo bado ndani ya CCM au Lowassa ambaye yuko nje ya CCM.
Njoo utueleze ni nani anaweza kupambana na ufisadi, ni Magufuli Mtuhumiwa wa Ufisadi wa Nyumba za Serikali ambaye amezungukwa na robo tatu ya wabunge waliotumia rushwa na uvunjaji wa maadili kupita kwenye kura za maoni au ni Edward Lowassa mtuhumiwa wa Ufisadi wa Richmond ambaye amezungukwa na wabunge waadilifu na wazalendo waliopita kwenye kura za maoni bila kuhonga wala kutoa rushwa nikiwemo mimi Mtatiro.
Na je baada ya CCM kuwapitisha watuhumiwa wa rushwa lukuki kugombea ubunge kwenye kampeni za mwaka huu bado utakipigia debe chama chako CCM?
Wala jazba hazihitajiki katika kujadili, tunahitaji hoja kwa wachangiaji wote, tusiwe wanafiki, kama unakula Nguruwe hebu kunywa na mchuzi wake, huwezo kujidai huli nguruwe huku unakunywa mchuzi wake "daily".
Leo nimepasua JIPU kama Malisa Godlisten!
                               Julius Sunday Mtatiro,
Dar Es Salaam.

No comments: