Baadhi ya waandishi wa habari za Michezo kutoka Vyombo mbalimbali vya habari, wanaounda timu ya Waandishi wa habari za Michezo Tanzania, Taswa Fc na Taswa Queens, wakimsikiliza Afisa wa Hifadhi ya Michael Ngatolu, wakati walipotembelea kwenye hiyo, walipokuwa katika ziara ya kuhitimisha Bonanza la 10 la Taswa Arusha lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
TIMU ya Taswa Fc na ile ya Taswa Queens, zinazoundwa na wachezaji wa Habari za Michezo kutoka vyombo mbalimbali vya habari Tanzania, jana ilihitimisha ziara yake ya siku mbili katika mikoa ya Arusha na Tanga.
Aidha timu hiyo ilifanikiwa kumaliza ziara hiyo bila kufungwa huku Taswa Queens, wakiibuka kidedea kwa kutwaa Ubingwa wa mashindano ya Bonanza la Taswa Arusha yanayofanyika kila mwaka, baada ya kuwagalagaza bila huruma timu ya Chuo cha Waandishi wa Habari cha Arusha AJTC kwa jumla ya mabao 37-3.
Wakati Taswa Queens ikitwaa Kombe hilo, Taswa Fc, wao walimaliza bonanza hilo bila kufungwa huku wakitoka sare katika michezo yake yote mitatu.
Katika mchezo wa kwanza Taswa Fc ambayo ilidhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, ilitoka sare ya bila kufungana na timu ya ORS ya Manyara, kabla ya kutoka sare ya bila kufungana tena na timu ya IMS Maji ya Chai, na baadaye kutoka sare ya bao 1-1 na timu ya Kampuni ya Habari Maalum ya Arusha.
Baada ya Bonanza hilo Taswa Fc, walielekea Tanga Segela na kucheza mchezo wake wa mwisho na timu ya Kombaini ya Segera na Michungwani na kuibuka washindi kwa mabao 2-0 katika mchezo uliokuwa mkali na wa kuvutia kutokana na timu zote kucheza kwa speed na kukamiana huku wachezaji wakionyesha uwezo wa hali ya juu.
|
No comments:
Post a Comment