Saturday, August 29, 2015

U-15, MORO KOMBAINI ZATOKA SARE


TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa 15 leo imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Moro Kids Uwanja wa Jamhuri, Morogoro katika mchezo wa kirafiki.

Katika mchezo mzuri na kuwasisimua, bao la U15 inayofundishwa na Bakari Shime lilifungwa na Alex Peter wakati la Moro Kids inayofundishwa na mchezaji nyota wa zamani nchini, Profesa Madundo Mtambo, lilifungwa na Boniface Joseph.  
Timu hizo zitarudiana kesho Saa 2:00 asubuhi Uwanja wa Jamhuri kabla ya kurejea Dar es Salaam na wachezaji kutawanyika kwa ajili ya kuendelea na masomo.
Timu hiyo inaandaliwa kwa ajili kucheza mechi za kufuzu Fainali za Vijana Afrika chini ya umri wa miaka 17 mwaka 2017 na kila wiki ya mwisho wa mwezi wamekuwa wakikutana kwa mazoezi na michezo ya kujipima nguvu.
Leo imekuwa mara ya kwanza timu hiyo kumaliza dakika 90 bila ushindi tangu waanze programu hiyo Juni mwaka huu, wakishinda mechi zote zao Mbeya na Julai Zanzibar. 

No comments: