Thursday, August 6, 2015

WAFANYAKAZI WA BENKI YA NBC WAFANYA KAZI ZA KIJAMII KATIKA SHULE YA MSINGI TOANGOMA

Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa Benki ya NBC, Alexander Mgowano (kushoto) akitoa mafunzo kuhusu ujasiliamali kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Toangoma, Kigamboni, Temeke nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya mpango wa wafanyakazi hao kujitolea muda wao kufanya shughuli za kijamii. Katika hafla hiyo iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Idara ya Uendedshaji pia walikabidhi madarasa matatu waliyoyafanyia ukarabati.

Ofisa Usimamizi wa Mikopo wa Benki ya NBC, Tausi Miller (kulia) akitoa mafunzo kuhusu ujasiliamali kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Toangoma, Kigamboni, Temeke nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya mpango wa wafanyakazi hao kujitolea muda wao kufanya shughuli za kijamii. Katika hafla hiyo iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Idara ya Uendedshaji pia walikabidhi madarasa matatu waliyoyafanyia ukarabati.  

 Ofisa Usimamizi wa Mikopo wa Benki ya NBC, Tausi Miller (wa pili kushoto) akikabidhi boksi lenye karatasi maalumu zinazotumiwa na watu wenye ulemavu wa macho kwa mwalimu Subira Rashidi (kulia) katika hafla hiyo.

Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa Benki ya NBC, Alexander Mgowano (katikati) akitoa zawadi kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Toangoma katika hafla hiyo. 

Meneja Usimamizi wa Mikopo wa Benki ya NBC, Mwanaisha Ayosi (katikati) akishikana mikono na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Toangoma, Victor Kangati, katika hafla ambayo wafanyakazi wa Idara ya Uendeshaji ya NBC walikabidhi madarasa matatu waliyoyafanyia ukarabati na pia waliwafundisha wanafunzi hao masuala ya ujasiliamali ikiwa ni sehemu ya mpango wa wafanyakazi wa benki hiyo kujitolea muda wao kufanya shughuli za kijamii. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo, Toangoma, Temeke nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana.

No comments: