Thursday, August 27, 2015

WLAC yawapiga msasa wanawake wagombea katika uchaguzi ujao


THEODOSIA MUHULO ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la WLAC akifungua warsha hiyo iliyoandaliwa na shirika hilo kwa ajili ya kuwakutanisha wanawake mbalimbali ambao ni wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu,warsha iliyokuwa na lengo la kuwapa uwezo zaidi ikiwa ni pamoja na kujiamini katika harakati za uchaguzi wa mwaka huu 

Mkurugenzi wa shirika la OXAFARM nchini Tanzania JANE FOSTER ambaye shirika hilo ndio wahusika wakuu na kama wadhamini wa harakati hizo za kujenga uwezo kwa makundi mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu,hapa akizungumza na wanawake mbalimbali ambao ni wagombea wa nafasi za ubunge kupitia vyama mbalimbali vinavyoshiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu,ambao walijitokeza kwa wingi katika warsha hiyo

Mmoja kati ya wawezezaji wa warsha hiyo FORTUNATA MAKAFU kutoka Dodoma akiendelea na kutoa mada mbalimbali katika warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es salaam

Wagombea mbalimbali waliojitokeza ambapo takribani wanawake 50 wameshiriki katika semina hiyo
Mgombea ubunge wa jimbo la Temeke kwa tiketi ya chama cha TLP mama NANCY MRIKARIA akizungumza na wanahabari nje ya ukumbi wa mkutano huo kuhusu changamoto mbalimbali ambazo zinawakumba wanawake wanaoshiriki katika uchaguzi huo ambapo amesema kuwa moja ya changamoto hizo ni swala la rasilimali Fedha za kutosha kufanya kampeni na maswala mengine katika uchaguzi 

Mgombea wa ubunge segerea kupitia chama cha mapinduzi CCM mama LUCY GEREMIA akizungumza na wanahabari waliotaka kujua manufaa ya mkutano huo kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu.

No comments: