Mkutano wa Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Soko la Majengo, Jimbo la Mtama, Mkoani Lindi leo Septemba 23, 2015 |
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Kalangalala mjini Geita leo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi, Dk. John Pombe Magufuli leo amehutubia mikutano katika miji ya Runzewe wilayani Bukombe, Katoro wilayani Chato na Geita mjini akiendelea na kampeni zake kwaomba wananchi kumpa kura za ndiyo ili aweze kuingia Ikulu ya Magogoni na kuwafanyia kazi watanzania kama kiongozi na Amiri Jeshi mkuu wa Tanzania.
Mgombea Urais Huyo amewaambia wananchi wa Geita kuwa mara atakapoingia Ikulu moja ya changamoto anazotarajiwa kuzipa kipaumbele cha kutatua, Ni pamoja na kuwapa maeneo wachimbaji wadogo wa madini nchini ikiwa ni pamoja na kuwakopesha mitaji na kuwapa vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi zao pamoja na mafunzo kwa ajili ya kuboresha uchimabaji wao ili uwe wa kisasa zaidi na kupandisha kiwango cha ufanisi wa kazi zao za uchimbaji madini .(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-GEITA)
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi kwenye kutano wake wa kampeni uliofanyika mjini Geita leo.
Picha mbalimbali zikionyesha umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo uliofanyika mjini Geita leo.
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza na Mjumbe wa kamati ya ushindi ya CCM mjini Heita wakati wa mkutano wa kampeni leo, kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Geita Mama Fatma Mwasa.
Mh. Temba kulia na Chege wasanii kutoka kundi la muziki wa kizazi kipya la TMK wakifanya vitu vyao katika mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika mjini Geita.
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akisikiliza kwa makini maelezo ya Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza na mjumbe wa Kamati ya ushindi Mh.Anthony Diallo huku Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Ndugu Abdallah Bulembo akisikiliza kwa makini.
Kundi la muziki la Yamoto Band nalo limefanya mambo makubwa katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza na mjumbe wa Kamati ya ushindi Mh.Anthony Diallo akiwahutubia wananchi wa mji wa Geita katika mkutano wa kampeni wa CCM katika uwanja wa Kalangalala.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita na mgombea ubunge wa jimbo la Geita vijijini Ndugu Joseph Kasheku Msukuma akihutubia katika mkutano huo na kuwaomba wananchi wa Geita kutopoteza bahati hivyo wampigie kura nyingi ili Dr. John Pombe Magufuli aweze kushinda kwa ushindi wa Sunami.
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea ubunge wa majimbo ya Busanda Mh. Rolencia Bukwimba na Dr Kalemani mgombea wa jimbo la Chato katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Katoro wilaya ya Chato.
Wananchi wakipunga mikono yao juu baada ya kufurahishwa na hotuba Dk John Pombe Magufuli mjini Katoro.
Picha zikiendelea kupigwa kwa staili mbalimbali katika mkutano huo.
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Katoro.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Ndugu Abdallah Bulembo akimkaribisha Dk. John Pombe Magufuli ili kuwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni mjini Katoro
Vijana wakiwa juu ya miti ili kupata ujumbe wa Dk. John Pombe Magufuli kwa ufasaha na umakini,
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili mjini Katoro wilayani Chato kwa ajili ya kuhutubia mkutano wa kampeni.
Wananchi wa Runzewe wilayani Bukombe wakiimba pamoja na Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano uliofanyika Runzewe.
Hapa ni Magufuli tu huku akionyesha dole gumba.
Vijana wa Runzewe wakiwa juu ya mapaa ya nyumba wakati Dk. John Pombe Magufuli akihutubia mkutano huo.
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi katika mji wa Nyakahura.
Kumbe hata watoto wanampenda Dk. John Pombe Magufuli kama wanavyoonekana katika picha hizi juu na chini.
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akienda sambamba na Mwanamuziki wa muziki wa Kizazi kipya Mwana FA aka Binamu.
MwanaFA akifanya vitu vyake jukwaani mjini Geita leo.
Wasanii mbalimbali wakipiga Push Ups jukwaani kuunga mkono kitendi alichokifanya Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli wakati alipopiga Push Ups jukwaani mjini Karagwe jana wamesema ni muhimu viongozi wetu wakawa na afya njema ili kutekeleza vyema majukumu yao lakini pia kuonyesha kuwa wanajali suala zima la kufanya mazoezi ili kuweka miili yao vizuri kiafya.
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akikumbatiana kwa furaha na kijana mlemavu wa ngozi Albino Lazaro Malendeka ambaye alikuwa mtumishi wa kikundi cha Red Briged cha Chadema baada ya kujiunga na CCM mjini Geita leo.
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwapokea mlemavu wa ngozi Albino Lazaro Malendeka kushoto ambaye alikuwa mtumishi wa kikundi cha Red Briged cha Chadema baada ya kujiunga na CCM mjini Geita leo na William Mabula Msalaba aliyekuwa mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Geita.
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwanadi wagembea ubunge wa mkoa wa Geita katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Geita leo.
No comments:
Post a Comment