TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini NEC imeshindwa kuzijibu tuhuma alizotoa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Tuhuma hizo ni zile za ubadilishaji holela kwa wakurugenzi ndani ya tume hiyo pamoja na Idara ya usalama wa Taifa kuhusika katika ufanyaji kazi pia kwenye tume hiyo.
Hayo yabainika leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano kati ya watu wenye ulemavu na NEC mkutano huo wenye lengo la kuwapatia uelewa kuelekea uchaguzi mkuu ambapo mara baada ya mkutano huo waandishi wa habari walimfuata Mwenyekitiwa NEC Jaji mstaafu Damian Lubuva ili kutaka kujua kuhusu madai hayo ya Mbowe.
Ambapo Jaji Lubuva amesema hawezi kujibu tuhuma hizo kwani ni za masuala ya utendaji ya kitume si vyema yakajibiwa.
“Jamani tumesema haya mambo ya utendaji wa kitume sio vizuri kuyazungumzia hadharani kwani yanaweza kuathiri utendaji wa kitume,si vema kuzungumzia”amesema Lubuva.
LUBUVA amedai kuwa hakuna haja ya kuanza kulalamikia wapishi walioko jikoni wakati chakula hakijaiva hivyo haoni haja ya kulalamika yanayotopkea tume na badala yake watanzania wawe na imani na kusubiri kazi nzuri ya tume hiyo
Waandishi wa habari walipombana na kutaka atolee ufafanuzi juu ya Mgombea wa Urais wa chama cha Mapinduzi CCM John Magufuli kutumia magari ya umma kwenye kampeni zinazoendelea,ndipo Jaji huyo akasema maswali hayo yote atayajibu kesho atakapokutana na wahariri wa vyombo vya habari.
kushindwa huku kwa tume ya uchaguzi kutolea ufafanuzi kunazidi leta msuguano baada ya hivi sasa kuibuka kwa taarifa za MKURUGENZI wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk. Sisti Cariah kuondolewa kinyemela kwenye nafasi hiyo.
Taarifa ambazo ,fullhabari, imezipata kutoka ndani ya tume hiyo zinasema mkurugenzi huyo teyari ameondolewa kwenye nafasi hiyo na haijulikana amehamishiwa wapi.
Hadi jana tovuti ya Tume hiyo hadi ilikuwa ikionyesha kuwapo mkurugenzi mmoja tu ambaye ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhan Kailima, huku ukiwapo unaosomeka kwamba kurugenzi nyingine zinaendelea kusukwa upya
Katika hatua nyengine Tume hiyo ya uchaguzi imetoa tamko kwa vyama vyote kwa kusema hakitasita kukichulia hatua kali chama ambacho kitatumia mda mwingi jukwaani kuwasema watu badala ya kunadi sera zake.
“Tumeviambia vyama vyote kufuata sheria ya uchaguzi ya mwaka 2015 kwa kuacha kutumia mda mwingi kujadili watu,bali tumewataka watangaze sera za chama husika na sio kutoa matusi jukwaani”amesema Lubuva.
No comments:
Post a Comment