Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Kinindoni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Camillius Wambura ameitaka jamii kushiriki katika uchaguzi mkuu
wa October 25, 2015 katika hali ya utulivu ili kukuza democrasia na kuwezesha
uchaguzi huo kuwa huru na wa haki.
Amesisitiza hayo katika kikao na wadau wa
uchaguzi kilichoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na asasi ya Hanns Seidel Foundation (HSF) uliofanyika
katika ukumbi wa maafisa wa Polisi Oysterbay, Kinondoni jijini Dar es Salaam
"Uchaguzi
huru na wa haki wenye kuzingatia democrasia
ni muhimu na hauepukiki kwani ni nyenzo muhimu katika kuandaa msingi
imara wa maendeleo ya taifa hili". alisema Kamanda
Wambura.
HSF na Jeshi la Polisi
waliandaa kongamano hilo kujadili ni
namna gani jamii iamasishwe kushiriki
katika ujao kwani uchaguzi wa kidemocrasia ni chachu ya maendeleo, na
endapo uchaguzi huo usipoendeshwa kwa umakini machafuko na vurugu vinaweza
kuibuka na hatimaye kuzorotesha maendeleo ya nchi hii.
Kongamano hilo
limeendeshwa kufuatia maboresho yanayoendelea ndani ya Jeshi la Polisi katika
mradi wake wa Polisi Jamii unaohusisha mashauriano, kutatua changamoto, pamoja
na mambo mengine. Aidha, hii ni fursa kwa Jeshi la Polisi kuwa na uelewa wa
pamoja na wadau wa uchaguzi na jamii kwa ujumla katika kubaini changamoto za
kiusalama, kijamii na kiuchumi ka kuweka mpango wa pamoja katika kutanzua
changamoto hizo.
"Ni fursa nzuri kwa wadau muhimu kama
viongozi wa madhehebu ya dini, vyama vya siasa, watu wenye ushawishi katika
jamii, na Taasisi zisizo za kiserikali: kuhimiza, kutia moyo, na kuonyesha
uhalali wa wajibu huo kuelekea huru na wa haki". amesema EMMANUEL MALILA - Mkurugenzi
Mtendaji wa TASODEMO (Taasisi inayojihusisha na uchambuzi wa masuala ya kisiasa
na Kijamii),
Aidha, kongamano hilo
limewawezesha washiriki kupata ufahamu juu ya masuala mbalimbali ikiwa ni
pamoja na haki za binadamu, mchakato wa uchaguzi mkuu, makosa ya uchaguzi, haki
na wajibu wa vyama vya siasa, sheria ya vyama vya siasa, mikutano ya hadhara,
vyama vya siasa katika chaguzi za kidemokrasia, kampeni sahihi, na madhara ya
watu kutokufuata sheria katika mchakato mzima wa uchaguzi mkuu.
The participants
lastly agreed with resolutions to be worked upon, which will be a catalyst to
community; the participants included: Assistant returning officers, religious
leaders, political parties leaders, Non-Governmental Organizations, Civil based
Organizations, Faith based Organizations, Influential personnel ,Law
enforcement organs, Media industry, Youth group (Bodaboda group) and Local
Government Authorities.
washiriki wa kongamano
hilo ni pamoja na viongozi wa madhehebu ya dini, viongozi wa vyama vya siasa,
taasisi zisizo za kiserikali, mashirika
ya kijamii, watu maarufu, vyombo vya ulinzi na usalama, wanahabari vikundi vya
vijana (bodaboda) na Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
No comments:
Post a Comment