Monday, September 21, 2015

Kampuni ya Fastjet kutoa mafunzo kwa maafisa wa viwanja vya ndege juu ya masuala ya wanyamapori

http://www.buyorsell.co.tz/wp-content/uploads/2015/08/fastjet...1.jpg

Kama sehemu ya mkakati wake wa kusaidia utoaji wa mafunzo kwa maafisa wa viwanja vya ndege,kampuni ya Fastjet Tanzania imeingia katika makubaliano na kampuni inayojihusisha na wanyamapori ya Uholanzi ijulikanayo kama AviAssist ambayo itatoa mafunzo kuhusu namna ya ulinzi wa wanyamapori kwa maafisa wa viwanja vya ndege.
 
Akizungumza na  vyombo vya habari, Meneja mkuu wa kampuni ya Fastjet ukanda wa Afrika mashariki Jimmy Kibati alisema kuwa, Fastjet itaendasha mafunzo haya katika ofisi zake za makao makuu jijini Dar es Salaam, huku akiongeza kwamba kozi itabeba sehemu ya wadau wote ambao uelewa na ushirikiano wao ni muhimu kwa utekelezaji kwa vitendo mpango wa usimamizi wa wanyamapori kwenye viwanja vya ndege.

Mafunzo yatafuata mwongozo wa kimataifa kwa muundo wake kutoka kwa mashirika ya ndege ya kimataifa na wadhibiti wakuu kama vile shirikisho la utawala la safari za anga marekani ," alibainisha Kibati.
 
Wakati wa kutangazwa kwa mkataba, ilionyeshwa kwamba licha ya ukarimu na vivutio vya wanyamapori vilivyopo katika ukanda wa Afrika Mashariki, uwepo wa wanyamapori ndani na nje ya viwanja vya ndege unaleta hatari kubwa na changamoto kwenye safari za anga.

Idadi ya viwanja vya ndege katika ukanda wa Afrika Mashariki zinakumbwa na hatari kubwa ya wanyamapori, kwa sehemu kwa sababu vinajikuta viko karibu na vyanzo vikubwa vya maji kama bahari,ziwa n.k au viko kwenye njia za kimataifa zinazotumiwa na makundi ya ndege kuhama sehemu moja kwenda nyingine. AviAssist husaidia viwanja vya ndege na mashirika ya ndege kuchukua hatua za awali katika kusimamia hatari ya wanyamapori katika viwanja vya ndega na maeneo ya karibu na viwanja vya ndege. Shirika linafanya bidii ili kuhakikisha usalama bora unakuwepo kwa wataalamu wa anga katika ukanda au karibu na nyumba zao.

Mashirika yote ya ndege ni lazima kuchukua hatua za kupunguza hatari, na ili kuhakikisha shughuli za viwango vya juu vya usalama, Fastjet inaendelea kushirikiana na wadau wa usalama wa anga, ikiwa ni pamoja na shirika la AviAssit, kukuza usimamizi wa usalama katika shughuli zetu" alisema Kibati.
 
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa AviaAsisst Tom Kok alisema kuwa, yeye ana matumaini kwamba shirika lake litawapatia Fastjet na washirika wake mafunzo bora zaidi na huduma bora ambazo wateja wanatarajia na wanastahili.
 
Tumefanya jitihada kupata mkataba huu, na mteja huyu mpya na tunajisikia fahari kwamba Fastjet imeichagua AviAssist kama mtoa mafunzo haya muhimu," alisema Kok.
 
Kok Aliongeza kuwa, mkataba huu kutoka kwa moja ya mashirika ya ndege mapya na yenye mhemko zaidi barani Afrika, inasisitiza kuongezeka kwa heshima ya soko ambalo AviAssist inalijenga katika bara la Afrika kwa ubora, gharama fanisi na utoaji wa wakati wa huduma za kuboresha usalama ambapo kwa sasa hakuna biashara mbadala ambayo ni yakinifu,”alisema.
 
Alielezea kwa kina kwamba,  shirika lake linatarajia kujenga biashara zaidi kwa ajili ya shirika, biashara ambayo kwa upande wake inasaidia  moja kwa moja bidhaa za AviAssist kama vile magazeti yetu ya bure yanayohusu usalama na makundi ya Facebook ya bure kwa wataalamu wa anga wa Afrika

No comments: