Rais wa Shirikisho la Mpira Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi anatarajiwa kukutana wazazi wa vijana wenye umri chini ya miaka 13 (U-13) waliochaguliwa kujiunga na kituo cha michezo cha Alliance kilichopo jijini Mwanza.
Malinzi anatarajiwa kukutana na wazazi wa vijana hao siku ya jumatatu ya tarehe 14, Septemba 2015 saa 5 kamili asubuhi katika shule ya Alliance, kabla ya taratibu za kuwakabidhi vijana hao kwa uongozi wa kituo hicho.
Mapema mwezi Juni mwaka huu TFF iliendesha mashindano ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 13 (U-13) yaliyofanyika jijini Mwanza, ambapo jopo la makocha liliweza kuchagua wachezaji 20 wenye vipaji ambao watajiunga na kituo hicho kwa ajili ya masomo ya kawaida na kufundishwa michezo.
Mpango huo wa kuwaweka vijana katika kituo cha Alliance una lengo la kuandaa timu bora ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17, itakayoshiriki kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana wenye umri huo zitakazofanyika nchini Tanzania mwaka 2019
|
No comments:
Post a Comment