Imeelezwa kuwa maeneo
ya masokoni,migodini na sehemu zenye matengenezo ya barabara ndizo sehemu
zinazoongoza kwa udhalilishaji wa wakiina mama hasa kwa njia ya matusi na
udhalilishaji wa kingono kwa wanamama hao.
Hayo yamebeinika leo jijini
Dar es salaam wakati wa Tamasha maalum lililoandaliwa na shirika lisilo la
kiserikali la EQUALITY FOR GROWTH (EFG) shirika ambalo linajishughulisha na
utetezi wa haki za kijinsia katika maeneo ya biashara tamasha ambalo limefanyika
katika soko la sterio Temeke jijini Dar es salaam kwa lengo la kutoa elimu kwa
watanzania wa eneo hilo juu ya unyanyaswaji wa wanawake katika maeneo ya
biashara na jinsi ya kuchukua hatua.
Katika kampeni
inayoendeshwa na shirika hilo iliyopewa jina la MPE RIZIKI SIO MATUSI ina lengo
la kupita katika mawnwo mbalimbali kutoa elimu kwa wafanya biashara hasa wakina
mama jinsi ya kuepuka mambo ambayo yanawadhalilisha wakiwa kazini na hasa jinsi
ya kutumia sheria ambazo zipo ili kujilinda na kadhia hiyo ambayo imetajwa
kuendelea kuenea katika maeneo mengi ya biashara hapa Tanzania.
Akizungumza wakati wa Tamasha
hilo Afisa Mradi wa kampeni hiyo ya MPE RIZIKI SIO MATUSI,Bi SUZAN SITTA
amesema kuwa maeneo ambayo tafiti za shirika hilo zinaonyesha kukithiri sana
kwa udhalilishaji wa wanawake katika maeneo ya biashara ni pamoja na maeneo ya
masoko,maeneo ya migodi,pamoja na maeneo ambayo kumekuwa kukifanyika shughuli mbalimbali
kama maeneo ya ujenzi wa bara bara.
Anaeleza kuwa
matusi,udhalilishaji wa kingono,kudharaulika ni moja ya kadhia nyingi ambazo
wamekuwa wakikutana nazo katika maeneo mengi ambayo shirika hilo limekuwa
likifanya ziara huku akikiri kuwa hali hiyo kuendelea kuwa kubwa kutokana na
kutokuwa na nia dhabiti ya kutoa elimu kwa wahusika juu ya tabia hiyo.
Wakazi waliohudhuria
katika Tamasha hilo la Temeke leo wamekiri kuwepo kwa maswala hiyo katika soko
la Sterio Jijini Dar es salaam ambapo wengi wao wamesema kuwa sababu kubwa ya
udhalilidhaji wa wanawake kazini unatokana na wanaume wengi kutokuwaheshimu
wanawake ambao wanafanya kazi mfano za mama Ntilie,wauza matunda,pamoja na
bishara nyingine katika soko hilo ambapo wameomba wahusika kuendelea kutoa
elimu pamoja na kuchukua hatua za kisheria.
Wadau mbalimbali wa kampeni hiyo wakiwemo pia wa wafadhili kutoka UN-GENDER wakiwa wanashiriki katika Tamasha hilo la kutoa elimu juu ya unyanyaswaji wa wanawake juu ya wanawake sehemu za Biashara |
Aidha wamesema kuwa
tabia hiyo inakuwa na madhara makubwa sana wa kwa wahusika ikiwa ni pamoja na
kushusha heshima zao,kutokujiamini wakiwa kazini,pamoja na kushindqwa kiufanya
biashara kwa kuhofia kadhia hiyo kuwakumba.
Shirika hulo limekuwa
liktimbelea maeneo mbalimbali ya masoko ambapo kwa lengo la kutoa elimu juu ya
unyanyaswaji wa wamnawake katika maeneo ya biashara na jinsi ya kujikinga na
kadhia hiyo
HAMAD JUMA mwenyekiti wa soko la STERIO TEMEKE akiiangumza na wakazi waliojitokeza katika Tamasha hilo |
Burudani ilikuwa ni sehemu ya kazi hiyo,Chinio unaweza kuangalia picha nyingi za tukio nzima leo |
No comments:
Post a Comment