Wednesday, September 30, 2015

Tigo yatoa mchango wa madawati 700 kwa shule za umma mkoani Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, (kulia) akimkabidhi madawati Kaimu Ofisa Elimu Mkoa huo, Gerald Kifyasi baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 700 yenye thamani ya Sh49milioni kutoka Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo leo.

Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Nyanda za juu Kusini Jackson Kiswaga akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi madawati.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Tigo nchini, Diego Gutierrez, (kushoto) akimkabidhi madawati yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, Tigo imetoa msaada wa madawati 700 yenye thamani ya 49 milioni kwa shule za msingi za wilaya za Rungwe, Mbozi na Mbeya Mjini.

 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, (kulia) akimkabidhi madawati Ofisa Elimu Shule za Msingi Jiji la Mbeya, Deusdedit Bimbalirwa, baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 700 yenye thamani ya Sh49milioni kutoka Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo leo.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro  (kulia) akiwa ameketi kwenye dawati na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Tigo nchini, Diego Gutierrez, mara baada ya kampuni ya Tigo kumkabidhi  mhe. Kandoro madawati 700 yenye thamani ya Sh49 milioni kwashule za msingi za wilaya za Rungwe, Mbozi na Mbeya Mjini .
Kampuni ya Tigo Tanzania kwa kushirikiana na shirika lisilokuwa la kiserikali linalotoa misaada katika jamii lijulikanalo kama Hassan Maajar Trust (HMT) wametoa mchango wa madawati 700 yenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni 49 kwenye shule za msingi 32  katika wilaya ya Rungwe, Mbozi na wilaya ya Mbeya Mjini.
 
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika moja ya shule jijini Mbeya, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez alisema: “ mchango huu ni sambamba na dhamira ya kampuni ya kuunga mkono mipango ya kijamii kupitia wigo wake wa kushirikisha jamii”.
 
“Kupitia mchango huu, kampuni ya Tigo inawajibika katika kutengeneza viongozi wa baadaye wakiwamo madaktari, wahandisi na wataalamu wengine wa nchi hii, "alisema Gutierrez.
 
Alisema, katika miezi ya hivi karibuni kampuni ilitoa mchango kama huo wa madawati katika mikoa ya Iringa na Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya ahadi ya dola za Marekani 50,000 kwa serikali, ahadi ambayo kampuni ya Tigo ilitoa mwaka jana ili kusaidia kukabiliana na uhaba wa madawati katika shule za umma nchini.
 
Tukio hili la makabidhiano pia lilihudhuriwa na Mwenyekiti wa shirika la Hassan Maajar Trust Bw xx ambaye aliishukuru kampuni ya Tigo kwa kusaidia mpango wa shirika hilo wa kukabiliana na uhaba wa sasa wa madawati katika shule za umma mkoani Shinyanga
 
 
Makabidhiano yalishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ambaye alisema madawati hayo700 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto katika wilaya hizo tatu, akitoa wito kwa wadau wengine wenye mapenzi mema kujitolea na kujiunga kwenye jitihada za kukabiliana na sehemu iliyobaki ya uhaba wa madawati mkoani humo.

No comments: