Baada ya waziri wa mambo ya nje Bernad Membe kuwapa tahadhari waangalizi
wa uchaguzi kutoka nje ya Tanzania kwa kuwataka kuwa makini na taarifa
watakazokuwa wanazitoa naye naibu katibu mkuu wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA MHh JOHN MNYIKAameibuka na kupinga kauli hiyo huku akisema kuwa hivyo vitisho na kamwe waangalizi
hao wazitishwe na badala yake wafanye kazi kwa kuzingatia weledi wa kazi yao
Mapema wiki jana Akizungumza na mabalozi kuhusu uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mapema
mwezi Oktoba mwaka huu, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,
Bernard Membe aliwataka waangalizi wa kimataifa
kutofungamana na upande wowote ambapo amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndiyo
yenye mamlaka ya kutoa taarifa na kusisitiza iwapo watabaini mapungufu yoyote
wanapaswa kupeleka kwa tume ya uchaguzi baada ya tume kutoa taarifa
Kauli hiyo mnyika
anasema ni mbinu za kuwapunguza nguvu waangalizi hao na kuwafanya washindwe
kupinga magoli ya mkono yatakayokuwa yanafungwa na chama cha mapinduzi katika
uchaguzi huo..
Habari24 tv imekuletea kauli za John mnyika tizama video hapo chini
No comments:
Post a Comment