Sunday, October 25, 2015

Mtiririko wa matukio ya uchaguzi kutoka waangalizi wa ndani TACCEO,leo siku ya kwanza


Wakati zoezi la upigaji na uesabuji kura nchini Tanzania likifanyika katika maeneo mbalimbali nchi nzima mtandao wa asasi za kiraia wa kuangalia chaguzi nchini wa TACCEO unaoratibiwa na kituo cha sheria na haki za binadamu nchini LHRC wamesema kuwa kwa ujumla zoezi hilo limeenda vizuri pamoja na changamoto ndogo ndogo zilizojitokeza katika vituo vya upigaji kura.


Katika Report yao ya kwanza iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Bi HELLEN KIJO BISIMBA imeeleza kuwa jumla ya waangalizi 1728 walioko mikoa yote nchini Tanzania wamereport zoezi hilo limekwenda kwa utulivu na amani huku wakisema kuwa zaidi ya asilimia 90%.ya vituo vilifunguliwa kwa wakati nchi nzima.

Waangalizi hao wamesema kuwa moja kati ya matukio ambayo waliyapokea kutoka katika maeneo mbalimbali ni pamoja na maeneo kadhaa zoezi la upigaji kura kuchelewa kuanza hadi saa sita mchana ambapo tukio hilo limetokea huko kimara stop over ambapo watu hadi kufikia saa sita walikuwa hawaajaanza kupiga kura.

Tukio nyingine ambalo limerepotiwa nna waangalizi hao ni sakata la mabox 6 ya kupiga kura yaliyokamatwa yaliyokamatwa yakiwa na baadhi ya vifaa vya kupigia kura katika maeneo ya Kilimanjaro kilema kati na makuyuni jimbo la vunjo.

Matukio yote hayo wamesema tayari wameyareport kwa tume ya taifa ya uchaguzi.

REPORT YA JIONI HII KUTOKA TACCEO

Bdo zoezi limeendelea vizuri kwa kiasi cheke ila maeneo mengine uchaguzi umeahirishwa kutoka huku kituo cha stop over kimara hadi kufikia saa kumi na nusu jioni vifaa vilikuwa havijafika na tume ilikuwa inaahidi kuwa imeagiza vifaa vipo njiani.

Jimbo la mkwajuni wilaya ya kaskazini A mkoa wa kaskazini unguja uchaguzi wa mgombea uwakilishi umeahirishwa baada ya kutokea mchanganyiko wa karatasi za kupigia kura hivyo wananchi waliendelea kupiga kura kwa nafasi nyingine za udiwani,ubunge,na Urais.

Katika kituo cha kujiandikisha cha SACCOS kata ya machanli wilaya ya chamwino jimbo la chilonwa baadhi ya wananchi wameshindwa kupiga kura kwa sababu majina waliyoandikisha kwenye daftari la kudumu ni tofauti na majina ambayo huwa wanatumia hivyo kuwekewa pingamizi la kupiga kura na mawakala wa vyama

Huko magu mkoani  mwanza karatasi zimechanwa zenye majina ya wapiga hura na watu wameshindwa kuona majina yao na limeleta usumbufu mkubwa.
Hadi sasa kuna vituo ambavyo vimemaliza kupioga kura na wanaendelea na zoezi la uhesabiji wa kura.

Katika kituo cha sasi kata ya Mbagata huko arumeru Magharibi vijana walikataa kuwapisha wazee kupiga kura kwa kisingizio kuwa wazee wataikchaguz chama cha mapinduzi.

Mkoani mbeya jimbo la Songwe Kituo cha shule ya msingi mkwajuni kata ya mwambani karatasi za kupigia kura kwa nafasi ya udiwani ziliisha na wananchi wakaendelea kupiga kura kwa nafasi ya urais na Ubunge hii leo.

ENDELEA KUFWATANA NASI KUPATA REPORT NyINGI ZAIDI ----

No comments: