Wakili Imelda - Lulu Urio Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC |
Mtandao wa Asasi za
Kiraia za Kuangalia chaguzi nchini jana ulipata pigo katika mwendelezo wake wa
kukusanya taarifa juu ya mchakato wa uchaguzi mkuu wa 2015 kama unavyoendelea
nchi nzima baada ya Jeshi la Polisi kuvamia kituo cha kukusanya taarifa
kilichopo katika ofisi za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ofisi ya Mbezi
Beach. Tukio hilo lisilo la kawaida lilitokea Majira ya saa nane mchana baada
ya polisi kufika kituoni hapo na kuwaweka wahusika wa kituo hicho wapatao 36
chini ya ulinzi na kuwashinikiza kusimamisha kazi na Kufungua mitambo bila
kutoa sababu ya kufanya hivyo.
Akizungumza na
waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC ambao ndio waratibu wa TACCEO Wakili
Imelda – Lulu Urio amelaani vikali kitendo cha jeshi la polisi kuvamia na
kusimamisha shughuli ambazo zinafanyika kwa mujibu wa sheria na pia zinafanyika
kwa kibali kutoka Tume ya Uchaguzi ya Tanzania.”Kitendo hiki ni cha kidhalilishaji
ukizingatia sisi( TACCEO) tunafanya kazi
kwa mujibu wa sheria na pia tuna vibali vya kufuatilia uchaguzi kwa mujibu wa
sheria” Kituo chetu kinaaminika kwa kufanya kazi kwa maslahi ya umma wa
Tanzania na hii sio mara ya kwanza kwa sisi kufuatilia uchaguzi za nchi hii
hivyo tumeshangazwa na kusikitishwa na kitendo hiki cha polisi kuvamia bila
taarifa” – Aliongeza.
Mkurugenzi wa Utetezi
na Maboresho wa LHRC Wakili Harold Sungusia akizungumza kwa masikitiko katika
eneo la tukio alisema “mpaka sasa hatujui kosa kwani tumekuwa tukifuatilia
chaguzi mbali mbali toka kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini na tumekuwa
tukifuata sheria na taratibu zote zinazopaswa kama waangalizi na hata Tume ya
Taifa ya Uchaguzi imetupa vitambulisho vya uangalizi kwa kutambua mchango na
nafasi yetu”.
Hata hivyo sakata hilo
bado linaendelea kwani wafanyakazi pamoja na vifaa vyao vya kazi ikiwemo
kompyuta 27 pamoja na simu zao za mkononi ambavyo vimeshikiliwa na Jeshi la
polisi likiongozwa na afisa mpelelezi wa Kituo cha Polisi cha Kawe aliyefahamika
kwa jina la Mgonja. Wafanyakaizi wamefikishwa Makao Makuu ya Polisi jijini Dar
es Salaam kwa uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment