Saturday, November 7, 2015

KOMBE LA SHIRIKISHO KUANZA KESHO


 Michuano ya Kombe la Shirikisho ya (Azam Sports Federation Cup) itafunguliwa rasmi kesho Jumapili (Novemba 8, 2015) kwa mechi tatu zitakazochezwa kwenye viwanja vitatu tofauti, ambao jumla ya timu 64 zitashirki kuwania nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.

Mechi rasmi ya ufunguzi itakuwa kati ya wenyeji JKT Rwamkoma ya Mara na Villa Squad ya Dar es Salaam itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
 Bingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Azam Sports HD ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.

No comments: