Friday, November 27, 2015

SERIKALI YAKANUSHA KUHUSU HAZINA KUACHWA TUPU

w1Kamishna wa Bajeti kutoka Wizara Fedha Bw. John Cheyo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu taarifa za upotoshaji zilizoripotiwa na vyombo vya habari hapa nchini kuwa hazina yakauka, taarifa hizo ni za upotoshaji kwani mfumo wa Serikali wa bajeti unaiwezesha Serikali kupanga vipaumbele vya matumizi kulingana na bajeti ilivyopangwa ambapo fedha zinazokusanywa kupitia mfuko mkuu wa Serikali ndizo hutumika. Kushoto ni Kamishna msaidizi wa Bajeti Bw. Immanuel Tutuba na kulia ni Mkurugenzi msaidizi Idara ya habari Maelezo Bw. Vicent Tiganya.
w2Kamishna wa Bajeti kutoka Wizara Fedha Bw. John Cheyo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu kubadilishwa kwa matumizi ya Fedha za Serikali ambazo zitaelekezwa kwenye shughuli zitakazowagusa wananchi ikiwemo uboreshaji wa sekta ya elimu ambapo awali fedha hizo zilipangwa kutumika katika sherehe za Uhuru na shughuli zisizo za lazima. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Idara ya Habari. (MAELEZO) Bw. Vicent Tiganya.
w3Kamishna msaidizi wa Bajeti Bw.Immanuel Tutuba akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu namna Serikali inavyokusanya mapato yake na kuyaingiza katika mfuko mkuu wa Serikali ili yaweze kutumika katika utekelezaji wa bajeti ya Serikali. Kulia kwake ni Kamishna wa Bajeti Bw. John Cheyo na kushoto ni msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma.
w5Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Fedha na vyombo vya habari ambapo Kamishna wa Bajeti kutoka Wizara hiyo Bw. John Cheyo alitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Serikali kulingana na mipango iliyowekwa katika kuwahudumia wananchi.

w6Kamishna msaidizi wa Bajeti Bw.Immanuel Tutuba akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam .Kulia nia Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma.
(Picha na frank Mvungi- Maelezo)
……………………………………………………………………………………………………
Na Jovina Bujulu-Maelezo
Dar es Salaam
Serikali imekanusha taarifa zinazosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa amekomba fedha hazina na kuiacha Serikali bila fungu lolote.
Hayo yamesemwa jijini dare es salaam na Kamishina wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha Bwa. John Cheyo huku akiwataka wananchi kupuuza habari hiyo kwani hazina ukweli wowote.

“Hazina inazo pesa za kutosha  na tunajivunia kufanya uchaguzi wa mwaka huu,  kununua mashine za BVR  kwa kutumia pesa za watanzania bila kutegemea msaada wowote kutoka nje ya nchi  na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka huu” alisema Bwa. Cheyo.

Pia aliongeza kuwa serikali imeendelea kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa bomba la gesi ambalo limekamilika hivi karibuni, vinu vya kuchakata gesi na ujenzi wa barabara nchini.
Aliendelea kusema kwamba mfumo wa serikali wa bajeti unaiwezesha serikali kupanga vipaumbele vya matumizi kulingana na bajeti ilivyopangwa ambapo fedha zinazokusanywa kupitia mfuko mkuu wa serikali ndizo hutumika.
Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa kipindi cha 2015-2016 ni shilingi Trilioni 22.5 na bajeti hiyo inatengenezewa mpango wa makusanyo na matumizi kwa kulipia mishahara ya wafanyakazi na miradi mbalimbali iliyoidhinishwa.
Pia katika matumizi mengine bajeti hiyo inalipia chakula cha wanafunzi, mikopo ya wanafunzi elimu ya juu, ununuzi wa dawa na vifaa tiba na chakula cha hifadhi ya taifa

No comments: