Kampuni ya simu ya Tigo imeomba
radhi wateja wake kutokana na kukatika kwa huduma zake katika sehemu nyingine
nchini jana.
Taarifa ya kampuni hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari
leo jijini Dar es Salaam imesema kukatika kwa huduma za Tigo “kulitokana na sababu
zilizo nje ya uwezo kwa kampuni zilizo tokana na kukatika kwa mkongo sehemu tofauti
tofauti.” Aidha taarifa hiyo iliendelea kusema kwamba “tatizo hilo sasa limeshughulikiwa
kikamilifu na huduma zote za Tigo zimerejea katika hali yake ya kawaida.’’
“Tuna sikitishwa na usumbufu uliojitokeza kutokana na
kukatika kwa huduma zetu natunapenda kuwahakikishia wateja wetu dhamira ya kampuni
yetu kuendelea kuwapa wateja huduma zenye ubora wa hali ya juu, za kutegemewa na
kwa gharama nafuu,” amesema Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez.
Aidha Gutierrez ametoa shukrani kwa wateja wa Tigo kwa
uvumilivu wao na kutangaza kwamba kama ishara ya kuomba msamaha kampuni ina wapa
wateja wake wote dakika 10 za muda wa maongezi, SMS za bure kwenda mtandao yote
na 10mb za kuperuzi Intaneti kwa siku nzima ya leo.Kifurushi hiki mteja ana kipata
kwa kutuma neno BURE kwenda namba 15304.
Mwisho
No comments:
Post a Comment