Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya VPO Sports Club, Nehemia Mandia, baada ya kuibuka na ushindi katika Bonanza maalum la kumuaga Dkt. Bilal, lililofanyika jana Nov 28, 2015 kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. VPO waliibuka kidedea baada ya kuwafunga timu ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa mikwaju ya penati 5-4. Picha na OMR
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula, akizungumza wakati wa Bonanza maalum la kumuaga Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, liliandaliwa na timu ya timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais (V.P.O Sports Club) lililofanyika kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete, uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam jana Nov 28, 205. Katika Bonanza hilo lililoshirikisha jumla ya timu Nne za VPO Sports Club, Wizara ya Mambo ya Nje, Kamati ya Amani waliochanganyika na Mabalozi na Amana Bank waliochanganyika na Zanzibar Fc, Timu ya VPO Sports Club iliibuka na ushindi kwa kuwafunga Mambo ya nje kwa jumla ya mikwaju ya penati 5-4 na kutwaa kombe la Bonanza hilo. Picha na OMR
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha kushiriki Nahodha wa timu ya Kamati ya Amani Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum, katika Bonanza maalum la kumuaga Dkt. Bilal, lililofanyika jana Nov 28, 2015 kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. VPO waliibuka kidedea baada ya kuwafunga timu ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa mikwaju ya penati 5-4. Picha na OMR
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha kushiriki Nahodha wa timu ya Mambo ya Nje, Christopher Mwitula, katika Bonanza maalum la kumuaga Dkt. Bilal, lililofanyika jana Nov 28, 2015 kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. VPO waliibuka kidedea baada ya kuwafunga timu ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa mikwaju ya penati 5-4. Picha na OMR
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na kutoa nasaha zake katika bonanza hilo la kumuaga rasmi katika utumishi wa umma.
Nahodha wa timu ya VPO Sports Club, Muhidin Sufiani, akimtoka beki wa timu ya Kamati ya Amani, Mhungaji Amos Nene, wakati wa Bonanza maalum la kumuaga Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, lililofanyika kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete,uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam jana Nov 28, 2015. Katika Mchezo huo VPO walishinda kwa bao 1-0 na kutinga fainali na Timu ya Mambo ya Nje ambapo pia waliibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya mchezo kumalizika bila kufungana. Picha na OMR
Nahodha wa timu ya Kamati ya Amani Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum, akimiliki mpira mbele ya beko wa VPO Sports Club, Kibiti wakati wa Bonanza maalum la kumuaga Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, lililofanyika kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete,uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam jana Nov 28, 2015. Katika Mchezo huo VPO walishinda kwa bao 1-0 na kutinga fainali na Timu ya Mambo ya Nje ambapo pia waliibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya mchezo kumalizika bila kufungana. Picha na OMR
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Nahodha wa timu ya VPO kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
………………………………………………………………………………………………….
Na Muhidin Sufiani, Dar
Timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, VPO Sports Club, jana Nov 28, 2015 imetwaa kombe la bonanza maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kumuaga rasmi Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kwa kuifunga kwa mikwaju ya penati 5-4 timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika mchezo wa fainali.
Katika bonanza hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Park (JMK Park) zamani Kidongo Chekundu, timu hiyo iliianza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kamati ya Amani Tanzania iliyoongozwa na Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum.
Baada ya mechi hiyo, Timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais ilicheza mchezo wa fainali dhidi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambayo ilimaliza katika nafasi ya pili, ilifuzu katika hatua hiyo baada ya kuifunga timu ya Amana Benki kwa mabao 2-1.
Katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu, timu ya Amana Benki iliifunga timu ya Kamati ya Amani kwa mabao 2-0. Makamu Rais Mstaafu Dk Bilal alishuhudia michezo yote hiyo na kukabidhi vikombe kwa washindi.
Akizugumza baada ya michezo hiyo, Dkt. Bilal, aliwashukuru waandaaji wa bonanza hilo kwa kumuaga rasmi na kusema michezo ina umuhimu mkubwa sana katika maisha ya kila siku ya binadamu ikiwa ni pamoja na kujenga afya, kuhimarisha na kuanzisha urafiki na vile vile kuburudisha.
“Nimefurahi sana kuona jinsi mlivyoonyesha ushindani mkubwa na vipaji vya hali ya juu, sikujua kama kuna wachezaji wazuri namna hii, nawapa pongezi sana na msiache kuandaa mabonanza mengine kama haya mara kwa mara, mnatakiwa kufanya kila mara ili kujenga afya zenu na kuanzisha na kudumisha urafiki na amani” alisema Dkt Bilal.
Aidha Dkt. Bilal alitoa wito kwa wanamichezo nchini kutumia uwekezaji huo mkubwa kutoka kwa Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete kuendeleza vipaji. “Hapa kuna viwanja vya mpira wa miguu, mpira wa kikapu, netiboli, mpira wa mikono, mpira wa wavu, tumieni fursa hii kwa ajili ya kuendeleza vipaji na kuiwezesha nchi kufanya vyema katika michuano ya Kimataifa,” alisema.
No comments:
Post a Comment