Thursday, December 3, 2015

Watanzania Washauriwa Kujenga Kizazi Kisichokuwa na Maambukizi ya UKIMWI- “Kufikia sifuri tatu

Dk. Nalin Nag Mshauri Mwandamizi wa madawa, aleji, upungufu wa kinga pamoja na magonjwa ya kuambukiza kutoka hospitali za Apollo; New Delhi.



Na Mwandishi wetu,
Siku ya UKIMWI duniani inaadhimishwa tarehe mosi desemba kila mwaka, kutoa fursa kwa jamii kuungana ulimwenguni kupiga vita gonjwa la UKIMWI, kuwapa moyo wale wote wanaoishi na virusi vya ukimwi na kuwakumbuka wote waliokufa kwa ugonjwa huu. Siku ya ukimwi duniani iliadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1988.

Zaidi ya miaka 30 toka ukimwi ulipoanza kusambaa nchini Tanzania, msisitizo umewekwa kwenye maendeleo ya mikakati na mbinu zaidi za kupunguza maambukizi na kuongeza huduma za matibabu. Kwa mwaka 2011, inakadiriwa watanzania milioni 1.6 walikuwa wanaaishi na virusi vya UKIMWI na miongoni mwao, milioni 1.3 ni wenye umri zaidi ya miaka 15, hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2012 kutoka shirika la umoja wa mataifa la kupambana na UKIMWI (UNAIDS). 


Licha maambukizi ya UKIMWI kwa Tanzania bara yamepungua kutoka asilimia 7.0 hadi 5.3 katika kipindi cha mwaka 2003/2004 mpaka 2011/2012 miongoni mwao wakiwa watu wenye umri wa miaka 15-49 na kutoka asiimia 6.3 mpaka 3.9 ambao ni wanaume katika kundi hilo, na hakuna takwimu nzuri za kuonyesha kupungua kwa maabukizi kwa upande wa wanawake.


Kwa mujibu wa TACAIDS taarifa za mwaka 2013, kwa tanzania bara maambukizi kimikoa yanatofautiana kutoka asilimia 1.5 kwa mkoa wa Manyara  hadi asilimia 14.8 kwa mkoa wa Njombe.

“Kufikia sifuri tatu”  ndio kauli mbiu iliyochaguliwa na kampeni ya siku ya ukimwi duniani kuadhamisha ya siku ya UKIMWI duniani kwa mwaka huu. Kwetu tanzania kupitia TACAIDS tunahamasisha “kufikia sifuri tatu” tukimaanisha “sifuri katika maambukizi mapya ya UKIMWI”, sifuri katika kuwanyanyapaa na kuwanyanyasa waathirika, na sifuri katika vifo vinavyohusisha UKIMWI”. Maudhui hayo yalipitishwa tokea mwaka 2011 yatumike mpaka 2015, yakitafsiri yale malengo ya UNAIDS ya kufikisha kiwango cha “kufikia sifuri katika maambukizi mapya ya UKIMWI”, na sifuri katika vifo vinavyohusisha UKIMWI”. 


Maamuzi ya kuchagua “kufikia sifuri tatu” yalifikiwa baada ya mahojiano ya kina na watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI, wanaharakati wa afya na taasisi ya kijamii.
Katika kuweka msisitizo katika maudhui ya mwaka huu, “kufikia sifuri tatu”, Dk. Nalin Nag mshauri mwandamizi wa madawa, aleji na upungufu wa kinga pamoja na magonjwa ya kuambukiza kutoka hospitali za Apollo; New Delhi  anawaasa watanzania kuepuka maambukizi mapya ya UKIMWI, kuepuka kunyanyapa waathirika wa UKIMWI katika familia na jamii zetu na ikiwezekana kufuta kabisa vifo visababishwavyo na UKIMWI.

UKIMWI ni kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wetu na tunaweza kupambana nacho kwa urahisi zaidi ya mashambulizi ya kigaidi yanayofanywa kwa kushtukizwa- “kufikia sifuri” katika maambukizi ya UKIMWI inawezekana kabisa kama wote tukidhamiria. Alisisitiza Dk. Nalin Nag
Mtazamo chanya katika maisha, ushirikiano kutoka katika familia na marafiki, malalamishi ya ukandamizwaji kutoka kwenye jamii kwa wingi wa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI ni tatizo la muda tu. Sheria kali zinahitajika kulinda na kutunza utu wa wahanga wa janga hili. Aliongeza Dk. Nalin Nag.

Dk. Nalin Nag anasisitiza kuwa wagonjwa UKIMWI wafanye vipimo vyote vya afya zao mara kwa mara, vipimo vya damu maabara, ufanisi wa ini, figo, kifua na tatizo la hepatitis B. magonjwa nyemelezi kama kifua kikuu, pneumonia na mengineyo yanatakiwa kudhibitiwa muda wote kabla ya kuanza kutumia dawa za ARV.

mlo sahihi, uongezaji wa kinga, mitindo ya maisha, na namna ya kupambana na msongo wa mawazo ni vitu vinavyojumuisha mlolongo wa kuboresha maisha bora kwa waathirika ambao kwa sasa wanatarajia kuongeza muda wa maisha yao kwa matumizi sahihi ya ARV. Alisema.

Dk. Nalin Nag anaelimisha jamii kuhusu umuhimu wa matumii ya dawa za ARV kwa waathirika wote wa UKIMWI. Hii imebadilisha kabisa makali ya ugonjwa na kuongeza ujasiri katika kutokomeza maambukizi mapya. Dawa tofauti za ARV zinapatikana na zinatumika zikiwa na kinga za aina 4 tofauti kwa ajili ya kudhibiti nguvu za virusi na kupunguza makali ya ugonjwa.

katika mazingira mengine huwa virusi havionekani kwenye damu hadi mwishoni mwa miezi sita hadi mwaka” aliongeza Dk. Nalin Nag kutoka Hospitali za Apollo Indraprastha.

Katika kitengo cha afya ugonjwa wa UKIMWI unabaki kuwa changamoto kubwa ulimwenguni, hasa kwa wananchi wenye kipato cha chini au cha kati. Na matokeo ya hivi karibuni kuhusu upatikanaji rahisi wa ARV, kumefanya wagonjwa wa UKIMWI kuweza kuishi maish marefu zaidi yenye afya bora. Kwa kuongezea, imedhibitishwa kuwa ARV inaepusha maambukizi endelevu ya UKIMWI.

UKIMWI umeendelea kuenea ulimwenguni, kwa mujibu wa taarifa za sasa za shirika la umoja wa mataifa la kupambana na UKIMWI (UNAIDS) takwimu za mwaka 2012, inakadiriwa watu milioni 34 wanaishi na virusi vya UKIMWI zaidi ya jinsi ilivyokuwa awali nah ii pia ni kutokana na matumizi ya dawa za ARV. Nchi zilizopo chini ya jangwa la Sahara zimebaki kuwa nchi zilizoathirika zaidi na janga hili la UKIMWI. Mwaka 2011, ilikadiriwa kuwepo kwa maambukizi mapya milioni 1.8 kwa nchi hizo; asilimia 69 ya watu wote wanaoishi na virusi vya UKIMWI wanapatikana katika nchi zilizopo chini ya jangwa la Sahara barani Afrika (UNAIDS, 2012).

No comments: