Mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es Salaam imefuta kesi iliyokuwa inamkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof.Ibrahim Lipumba na wenzake 30.
Mwendesha mashtaka wa serikali amewasilisha hati mahakamani hapo inayoeleza kuwa mwanasheria mkuu wa serikali hana nia tena ya kuendelea kesi hiyo.
Profesa lipumba na wenzake 30 walikuwa wameshtakiwa kwa kosa la jinai la kufanya mkusanyiko usio halali kwa mujibu wa sheria za nchi mnamo januari 22 na 27 maeneo ya Temeke jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment