Thursday, December 3, 2015

Lukaza Blog yaleta Tunzo Nyumbani. Asanteni Wasomaji, watembeleaji na Bloggers wenzangu

Mmiliki wa Lukaza Blog, Josephat Lukaza akiwa ameshikilia Tunzo aliyoshinda katika Kipengele cha Blog Bora ya Siasa katika Shindano la African Blogger Awards 2015 lililofanyika nchini Africa Kusini .Tutembelee kwa kufuata link hii http://www.josephatlukaza.com
Shindano la African Blogger Awards linaloendeshwa na Kampuni ya Webfluential ya Nchini Afrika Kusini lilianzishwa mnamo mwaka 2014 huku Lukaza Blog ikishiriki Kwa Mara ya Kwanza na kuibuka kuwa mshindi wa Pili wa Blog bora ya Kuelimisha kwa mwaka 2014.

Kwa Awamu ya Pili ya Shindano la African Blogger Awards liliofanyika mwaka 2015 Lukaza Blog pia iliweza kushiriki katika Vipengele vitatu huku ikiibuka Mshindi katika Kipengele Kimoja tu cha Blog Bora ya Siasa ambapo ushindi huo ulitangazwa tarehe 5 May 2015 kupitia Kurasa ya Twitter ya African Blogger Awards.


Katika Kinyanganyiro hiko Cha African Blogger Awards nilikua nikichuana na bloggers wengine kutoka Mataifa mbalimbali ya Africa na kuweza kuwagaragaza na hatimaye kuibuka Mshindi wa Kipengele cha Blog bora ya Siasa huku mshindi wa Pili akitokea Afrika Kusini.

Uendeshaji wa Shindano hili ulifanyika kwa kutumia njia ya Kitaalamu zaidi ijulikano kama Impartial Judgement ambapo hakuna kupiga kura wal kutaja jina la blog bali ni mfumo wenyewe wa mtandao ndio unaoweza kutoa majibu.

Ni mara ya Kwanza kabisa nchini Tanzania Mmiliki wa blog ya Lukaza, ndg Josephat Lukaza kuweza kuleta tunzo kutoka Kwenye mashindano yanayohusu blogs ambapo Kwa Tanzania hakuna shindano lililowahi kufanyika Wala kuandaliwa zaidi ya mashindano kama hayo kufanyika Nchi nyingine Duniani.

Sisi Kama Lukaza Blog tunajivunia kuibuka na Ushindi huu ambapo Kiukweli umetupa changamoto sana na kutuonyesha kuwa kumbe Blog zetu hata nje ya nchi zinatembelewa na zina wapenzi wengi sana lakini pia imetupa hali ya kujituma zaidi na zaidi na kuhakikisha tunafanya kile tunachoweza kuhakikisha tunaipasha Dunia kuhusiana na kile kitokeacho Duniani, Hususani Tanzania.

Lukaza Blog imeweza kuandika historia kwa kushinda katika shindano hilo la Africa Blogger awards na kufanikiwa kuleta Tunzo Nyumbani.
Tunzo hii iwaendee Wasomaji wangu wote kwa maana bila nyie Lukaza Blog isingeweza Kunyakua tunzo hii katika Shindano la African Blogger Awards lililomalizika Mnamo mwezi May 2015 huko Afrika ya Kusini. Lukaza Blog iliweza Kuibuka Mshindi wa Kwanza katika Kipengele cha Blog Bora ya Siasa na kuwashinda wapinzani wake ambapo Mshindi wa Pili akiwa ni Blogger kutoka Afrika Kusini.

Vilevile Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana wafuatiliaji wa Lukaza Blog kwa sapoti yao kwangu na timu nzima kwa maana Mafanikio haya Madogo tu yaliyopatikana wao pia wamehusika.
Shukrani zangu za Dhati kabisa Ziwaendee pia Bloggers Wenzangu Kiukweli Ushirikiano wao Kwangu napo kumeongeza tija na msukumo wa hali ya juu katika Kushinda tunzo hii hatimaye Tunzo hii imekuwa sio ya Lukaza Blog tu bali ni Kwa Tanzania Nzima na Watanzania Wote.

Asanteni sana na hapa sio mwisho tunaendelea kupambana na Changamoto ambapo sisi kama Lukaza Blog kwetu changamoto ni nafasi ya mafanikio.
Asanteni sana Bloggers, Wasomaji, Taasisi za Ndani ya Nchi na Hata Barclays Africa kwa kuona tija na kutuamini Lukaza Blog Kuweza Kufanya kazi na Nyinyi kwa Kipindi chote cha Miezi Sita kuanzia July hadi December yote hii ni njia ya kuelekea Kwenye kilele cha Mafanikio huku Juhudi, Heshima, Busara na ushirikiano vikitawala kichwa kwangu.

Tunzo hii ni heshima pia Kwetu Tanzania kwasababu tumeanza kuonyesha Dunia kuwa na Sisi Tupo tumeanza kwenye Muziki, Filamu na Sasa ni Blogs. Pia unaweza kututembelea kwa Kubofya hapa

No comments: