Friday, December 18, 2015

Mvua yaathiri Shule huko Masasi

Kushoto ni mbunge wa jimbo la ndanda CECIL MWAMBE akiangalia nadarasa yaliyoezuliwa kwa upepo wa mvua (Picha na Haika Kimaro)
Haika Kimaro
Masasi.Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimesababisha mvua iliyoambatana na upepo mkali kuenzua madarasa matatu na ofisi ya walimu katika shule ya msingi Mlingula kata ya Mlingula wilayani masasi na kuacha kuacha hali ya madarasa katika hali mbaya hapo juzi.
Wakizungumza na gazeti hili shuleni hapo mmoja wa wazazi wanaosomesha watoto shuleni hapo,Kauli Hamis alisema kuwa hali hiyo imewarudisha nyuma kimaendeleo kwani wanalazimika kuanza ujenzi wa madarasa mapya badala ya kujenga.
 Mwalimu wa shule hiyo ambaye ni mwenyekiti wa ujenzi mwalimu Mussa Chitama akizngumzia tukio hilo
“Athari iliyotukumba ni kubwa madarasa yamebaki machache kwahiyo inatulazimu kuanza ujenzi wa madarasa upya badala ya kufanya kazi zingine lakini tunashukuru wakati yanaezuliwa wanafunzi walikuwa tayari wapo likizo,”alisema Ally
Naye Mikidadi Ally alisema kuezuliwa kwa madarasa hayo imekuwa pigo kwao kwani ifikapo Januari watoto watashindwa kusoma endapo ujenzi utakuwa haujakamilika.
Mkazi wa eneo hilo
“Hili ni pigo maana ifikapo Disemba watoto wanarudi kusoma madarasa yakiwa hayajakamilika watalazimika kukosa masomo,”alisema Ally
Akizungumza mbunge wa jimbo la Ndanda,Cecil Mwambe baada ya kutembelea shule hiyo kujionea athari aliwataka wananchi kujitoelea nguvu kazi kwaajili ya kufyatua matofali na kuahidi kutoa mifuko 200 ya saruji ili kujenga madarasa mapya kutokana na yaliyopo kuonekana kuwa chakavu.

“Kwanz anitoe pole,nitaonana na mkurugenzi pamoja na msimamizi wa elimu kuona tunatua vipi hili tatizo lakini niwaombe wananchi kujitolea nguvu kazi kwa kufyatua tofali na mimi nitaleta saruji mifuko 200 ili tujenge upya madasa kwani haya yaliyopo yanaonekana sio rafiki kwa watoto kutokana na yenyewe kuonyesha dalili za kudondoka na  nyufa ambazorunaziona,”alsiema Cecil Mwambe

 Hata hivyo mwalimu wa shule hiyo amabye ni mwenyekiti wa ujenzi mwalimu Mussa Chitama pamoja na mtendaji wa kijiji,Exevia Msewe alisema tayari wananchi wamekubaliana kwa kila kaya kuchangia fedha kiasi cha Sh 2500 ili kuanza ujenzi mara moja kabla wanafunzi hawajafuangua shule hapo Januari mwakani.

Hata hivyo madarasa mengine yaliyosalia yalionekana kutokuwa salama kwa wanafunzi kutokana na kuwa yalijengwa miaka ya zamani kwa tofali za udongo.

No comments: