Tuesday, December 1, 2015

Tigo yazindua huduma ya 4G Dodoma

Watoa huduma wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, wakisajili line za simu za wateja waliohamia katika huduma mpya ya 4G LTE wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo mjini Dodoma jana.

Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akimkabidhi zawadi ya modem mshindi wa bahati nasibu Romanus Chuwa.


Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa Mkoa wa Dodoma Luteni mstaafu Chiku Ghallawa (katikati) akishirikiana na wageni maalum kupiga ngoma ikiwa ni sihara ya uzinduzi rasmi wa huduma ya 4G LTE uliofanika jana mjini hapa.

 Mkuu wa mkoa wa Dodoma Chiku Ghallawa akipatiwa maelezo kuhusu router jinsi inavyofanya kazi, mgeni rasmi huyo alitembelea banda la wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, mara baada ya kuzindua huduma mpya ya 4G LTE jana. 
 Wadau waliohudhuria uzinduzi wa huduma ya 4G LTE wakifuatilia kwa makini wakati wa uzinduzi huo.

No comments: