Na Mwandishi Wetu
Kwa mara nyingine tena na kama ada ya kila mwaka katika kipindi hiki, sikukuu ya Krismasi inakaribia. Kama yalivyo mazoea mihemko na kelele za kadi za sikukuu yatakuwapo ila tofauti na zamani, barua, kadi za sherehe za Krismasi n.k sio tena jambo lakujivunia. Wakati jamii ikiwa inafikiria kuhusu hadhi yake kiuchumi na kijamii kutokana na kukabiliwa na mabadiliko, hadhi ya mtu binafsi pia imekuwa inaangaliwa. Hivyo ndivyo vipaumbele.
Kwa baadhi ya watanzania hivi sasa licha ya mahitaji muhimu ya binadamu ambayo ni chakula, malazi, mavazi, huduma za afya na elimu kipaumbele kinachofuata ni kuwa na simu ya mkononi. Hali hiyo inatokana na sababu njia za mawasiliano zilizozoeleka kama barua simu za kawaida za nyaya zimeanza kutoweka kwa kasi.
Hata hivyo baadhi ya vitu havitabadilika inawezekana kusema hivyo angalau kwa muda mfupi ujao. ‘Makazi asilia’ kwa kuzingatia mazingira ya kiafrika siku zote yatabakia kuwa hivyo na ndio maana watanzania wengi wanaoishi mjini nyakati za sikukuu husafiri kuelekea majumbani mwao kwa ajili ya kusherehekea tukio hili la mwaka na wapendwa wao na marafiki wakiwa wamewachukulia zawadi.
Kwa hiyo kufanya manunuzi ya zawadi kwa ajili ya ndugu kunaweza kuwa shughuli ngumu, lakini hilo halimaanishi kuwa kuibuka na wazo la kufikiria zawadi ni jambo lililoepukikika kutoa zawadi kwa kila mtu bila kujali jinsia zao au umri.
Watu wanatafuta mbali na kwa mapana, wakijaribu, wakionja na kutafuta aina ya zawadi za Krismasi kwa ajili yao na wapendwa wao ikiwa ni kuwapatia zawadi nzuri na ya kipekee.
Kwenye enzi hizi za kidijitali njia mbadala ni nyingi kwa wale wanaotafuta zawadi itakayodumu kwa muda mrefu kwa wapendwa walio na uelewa wa teknolojia itakuwa vipi kuwepo kwa ongezeko la mawasiliano ya simu za mkononi hata kwenye maeneo ya ndani vijijini ambako mwandishi wa makala haya ana bibi yake mzee wa miaka 90 na ana simu ya mkononi!
Kwa mujibu wa mamlaka ya usimamizi wa mawasiliano Tanzania(TCRA) hivi sasa watumaiji wa simu za mkononi wanafikia milioni 32 ambao ni sawa na asilimia 67 ya idadi ya watu wake milioni 45 na idadi hiyo inaongezeka kwa kasi.
Katika hali hiyo zawadi ya Krismasi ikiwa ni simu ya mkononi inashauriwa kuwa ni zawadi nzuri ambayo mtu anaweza kununua kwa ajili ya mpendwa wake au ndugu katika msimu huu. Ni zawadi ya thamani hata baada ya aliyetoa atakapokuwa amerudi mjini. Kama simu hiyo ya mkononi itakuwa ni simu ya kisasa yaani Smartphone hiyo itakuwa ni sifa ya ziada kwa kifaa hicho.
Simu za mkononi zenye ubora wa juu zikiwa na muda wa ziada wa maongezi pamoja na vifaa vya simu ya kisasa (Smartphone) ni chaguo lenye haiba ya zawadi ambalo litaifanya mioyo ya wapokeaji kudunda kwa kasi wakiwa na furaha. Angalau hicho ndio mwandishi huyu alikigundua baada ya kufanya manunuzi kwenye duka la Tigo lililopo Mlimani City hivi karibuni.
“Wateja wananunua zawadi za simu haraka kuliko ilivyozoeleka. Aina zote za simu zinanunuliwa haraka hususan aina ya Tecno. Kama unavyoona tutalazimika kuleta mzigo mwingine kwa ajili ya mauzo ya kesho,” anasema Linda ambaye ni muuzaji kwenye duka la Tigo la Mlimani City, Dar es Salaam.
Kwa kiasi cha shilingi 99,000 mtu anaweza kupata simu aina ya Tecno Y3+ inayotumia kadi mbili za simu ikiwa na skrini ya kugusa, kamera mbili na kumbukumbua ya GB8 ikiwa pia na MB512 na betri yenye uwezo maradufu (2800mAh) ofa ambayo inavutia na wengi wanaoishi mjini wanaimudu kwa ajili ya kuchukua zawadi ya kumbukumbu kwa ndugu wakati wa msimu wa sikukuu.
Hali kadhalika kama ipo fursa ya kifedha kuna zawadi nyingine kwenye ofa hii. Hizi ni pamoja na Huawei Ascend Y625 ikiwa na muda wa maongezi wa shilingi 10,000, GB 4 za intaneti na muziki wa bure kwa mwezi kwa kiwango cha shilingi 225,000 tu pamoja na Samsung Galaxy J1 ya kiwango cha juu kwa kiwango cha 250 ikiwa imeunganishwa jumla na huduma ya 4GLTE yenye GB 30 za intaneti.
Idadi ya ofa za Tigo inaendelea kwa sababu ofa inaweza kuwa tamu zaidi kwa kuwa mtu anaweza kununua ZTE Kiss 3, na kuondokana na na kifaa cha kuhifadhi nishati kwa ajili ya simu.
Facebook ya Kiswahili
Kutokana na ukweli kuwa Watanzania wengi hutumia Kiswahili kama lugha mama ya mawasiliano, Tigo imeshirikiana na kampuni ya Facebook kutoa zana na nyenzo nyingine katika lugha hiyo. Hili hakika litakuwa ni kitovu cha kuuza na zawadi iliyofungwa ndani ya lugha ambayo wengi wanaielewa, ikiwa ni zawadi sahihi hususani kwa wale ambao wanahitaji uelewa wa lugha ya Kiingereza.
Hii ni mara ya kwanza kwamba huduma ya Facebook inakuwa ya bure na katika lugha ambayo watu wengi wanaielewa kwenye mtandao wa simu Afrika Mashariki.
Ushirikiano huo unamaanisha kwamba wateja wa Tigo wanaweza kwa mara ya kwanza, kutumia facebook kwenye simu zao bila kuingia gharama za data na kuunganishwa na watumiaji milioni mbili kwenye mitandao ya kijamii na Facebook yenye watumiaji bilioni 1.2 duniani kote.
No comments:
Post a Comment